Hali ya Uripoti wa Habari Tanzania 2022 (Utafiti wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam)

Hali ya Uripoti wa Habari Tanzania 2022 (Utafiti wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam)

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
3,984
Reaction score
13,760
Utangulizi 1.0 Utangulizi Tangu kuzinduliwa kwa ripoti kamili ya Mradi wa Ubora wa Vyombo vya Habari Tanzania “Yearbook on Media Quality in Tanzania” mwaka 2018, tayari ripoti tatu zimeshachapishwa.

Ripoti zote tatu, zimeelezea kwa kina ubora wa uripoti wa habari nchini na kwa hiyo ripoti hizo zinaweza kutumika kama rejea pekee zilizopo kuhusu ubora wa uripoti wa habari nchini Tanzania.

Ripoti ya mwaka huu imeendelea kuchunguza ubora wa uripoti kwa kuangalia aina tatu za vyombo vya habari – vinavyomilikiwa na serikali, vinavyomilikiwa na taasisi binafsi na vituo vya redio vya mikoani.

Ili kurahisisha usomaji na kwa kuzingatia mahitaji ya wadau wa habari ambao ama wanafanya kazi kwenye kundi fulani la vyombo vya habari (redio, magazeti na televisheni), au wenye maslahi na kundi fulani la vyombo vya habari, ripoti hii imeyawasilisha matokeo ya utafiti katika sehemu nne: muhtasari unaotoa picha ya jumla ya matokeo ya utafiti, matokeo ya magazeti, redio na televisheni.

Tofauti na ripoti zilizotangulia, ripoti hii imejumuisha sehemu mahsusi inayoangazia ubora wa uripoti wa habari visiwani Zanzibar. Ripoti kamili inapatikana kupitia ukurasa huu: (University of Dar es Salaam School of Journalism and Mass Communication (UDSM-SJMC) – Yearbook on Media Quality in Tanzania).

2.0 Muktadha wa vyombo vya habari Tanzania Mpaka kufikia mwezi Aprili 2022, kulikuwa na vituo vya redio 210, vituo 56 vya huduma za utangazaji, na magazeti na majarida 284 kwa Tanzania bara. Kwa mujibu wa takwimu za Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) , hadi kufikia mwezi Agosti, 2020, idadi ya watoa huduma za maudhui mtandaoni ilikuwa 575. Watoa huduma za maudhui mtandaoni hujumuisha blogu za mtandaoni, majukwaa ya mtandaoni, redio za mtandaoni, Televisheni za mtandaoni, na huduma nyingine za mtandaoni.

Umiliki wa maudhui mtandaoni unazihusu taasisi za kiserikali, mashirika yasiyokuwa ya kiserikali, makampuni, taasisi za mafunzo na utafiti na taasisi za kidini. Wamiliki wengi ni taasisi zisizokuwa za habari. Tasnia ya habari Zanzibar pia inaendelea kukua.

Kwa mujibu wa Tume ya Utangazaji Zanzibar (ZBC), visiwani humo kuna zaidi ya taasisi 50 za utangazaji na huduma za habari mtandaoni ambazo tayari zimeshasajiliwa.

Umiliki wa vyombo vya habari vya uchapishaji, kwa sehemu kubwa unatawaliwa na magazeti yanayomilikiwa na serikali—Zanzibar Leo, Zanzibar Mail, Zaspoti, na Zanzibar Leo Wanawake. Ni Fumba Times pekee, gazeti la mtandaoni lililoanzishwa Juni 2019 , ndilo gazeti binafsi linalochapishwa Zanzibar.

===================

Hali ya uripoti kwa mada
Vyombo vya Habari Nchini Tanzania huandika kuhusu mada mbalimbali, masuala ya Maendeleo (elimu, afya, kilimo, mazingira, maji) yameonesha kuripotiwa zaidi (Asilimia 30)

Masuala tete (migogoro, matatizo ya kijamii, rushwa, utawala bora, ukatili wa kijinsia kwa asilimia 25 masuala ya kiuchumi (miundombinu, mafuta na gesi, ajira, biashara) Asilimia 22.

Masuala ya kisiasa yamepewa nafasi ndogo yakiwa na Asilimia 10 ya uripoti wote, na masuala yanayohusu utafiti yameripotiwa kwa kiasi kidogo mno na Vyombo vya Habari (1%).

Vyombo vya habari vinaandika zaidi kuhusu maendeleo kwa kuwa ndio mada kuu inayobebwa na maofisa na viongozi wa serikali.

Kwa kuwa uripoti wa Vyombo vya habari kwa kiasi kikubwa unategemea taarifa rasmi zinazotolewa na viongozi hawa, hivyo, uwezekano wa masuala hayo kupewa kipaumbele na vyombo vya habari unakuwa mkubwa.

Kwa upande mwingine, masuala ya kisiasa yameripotiwa kwa uchache kwa sababu kwa sasa pamekuwa na shughuli chache za kisiasa nchini.

Hata hivyo, mijadala ya kisiasa imekuwa ya kudumu kwenye majukwaa ya mitandaoni kama vile Twitter Space na Clubhouse.
Moja.png

Habari za Ukosoaji wa Serikali zinaongoza katika taarifa za ukosoaji
Vyombo vya Habari vinapaswa kulinda Utawala Bora na kufuatilia Uwajibikaji wa Umma. Namna mojawapo ya kulitekeleza hili ni kutoa maoni yanayokosoa Watendaji mbalimbali ndani ya jamii.

Tofauti na ripoti zilizotangulia ambazo zililiangazia suala la maoni yenye ukosoaji kwa Serikali tu, uchambuzi wa Mwaka 2022 unakwenda zaidi ya hapo mpaka kwa Wadau wengine kama vile sekta binafsi, mashirika yasiyokuwa ya Kiserikali, Taasisi za kidini na mengineyo.

Matokeo ya utafiti yanaonesha Asilimia 4 tu ya kazi zote za Kihabari zilizochunguzwa ndizo zilizotoa maoni kosoaji kwa Serikali.

Mbili repo.png

Zanzibar: Mada zilizoripotiwa zaidi na Vyombo vya Habari
Ripoti ya Utafiti ya Hali ya Uripoti wa Habari Tanzania 2022 iliyofanywa na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) upande wa Zanzibar ilichukua sampuli 370 ya kazi za kihabari zilizochukuliwa kutoka Zanzibar Leo, Zenji FM, ZBC Radio, Micheweni FM, Hits FM na ZBC TV



Mada zilizoripotiwa Kama ilivyo kwa Tanzania Bara, uripoti wa vyombo vya habari Zanzibar ulitoa kipaumbele kwa masuala ya kimaendeleo kama vile elimu, afya, kilimo, mazingira, na maji (31%), vikifuatiwa na masuala tete (migogoro, haki za binadamu, matatizo ya kijamii, rushwa, utawala bora 27%), na masuala ya kiuchumi (19%).

Maeneo haya matatu ndiyo yameonekana kupendwa na vyombo vya habari. Pia yanaakisi nini viongozi wa kiserikali, ambao ndio vyanzo vikuu vya taarifa kwenye vyombo vya habari, wanaangazia. Kwa mara nyingine tena, kama ilivyo kwa wenzao wa Tanzania Bara, vyombo vya habari Zanzibar vimeupa uzito mdogo uripoti wa masuala ya kisiasa, jambo hili linaweza kuhusishwa na uwepo mdogo wa shughuli za kisiasa visiwani humo.

Hata hivyo, majukwaa ya mitandaoni kama vile Twitter Space na Clubhouse yanaendesha mijadala kuhusu siasa za Zanzibar.
Zanzibar Data.jpg
 

Attachments

Back
Top Bottom