Hali ya Usafiri wa Mwendokasi Mbezi Luis asubuhi ya leo ni shida kama zote

Hali ya Usafiri wa Mwendokasi Mbezi Luis asubuhi ya leo ni shida kama zote

Samahani jamani kwa kutoka nje ya mada Hv yule mwanamziki pale mbeya aliimba viongozi wananatuona sisi nyani alishafungwa au bado. Mwanamziki mjinga sana yule. Anatukana viongozi wetu.
Babake walishampiga mvua tatu. Yeye sijui labda kesi bado ipo mahakamani 😁
 
Naomba mheshimiwa Rais anipe ukuu wa hili shirika niendeshe,probation miezi 12,akiona sina ufanisi anirudishe ninapofanya kazi na anishushe pia;

Kuna shida nchi hii zinatengenezwa tu na watu wachache!
Hutaweza....

Sana sana ukizembea system itakuondoa na tunaimba 🎶🎶parapanda italia parapanda🎶🎶 mapema tu 😁
 
Na tena kibaya hao wapigaji Serikalini wanapeleka hela kwa mishangingi ya mjini. Wanawajengea mijengo na hela za kutanulia
 
Ndugu zangu wana JF hii video ni ya leo asubuhi katika Kituo cha Mabasi ya Mwendokasi Mbezi Luis, yaani kimekuwa na changamoto ya uhaba wa magari asubuhi ya leo Oktoba 16, 2023.

Foleni imekuwa kubwa ya abiria kusubiri mabasi, wapo ambao wamelazimika kusubiri mabasi hayo kwa saa tatu.

Upande wa Mabasi ya Mwendokasi yanayotokea Kibaha pia kulikuwa na abiria wengi kwenye vituo, mabasi ni machache na hivyo kusababisha msuguano wakati wa kuingia ndani ya usafiri huku baadhi yakipata tabu mlango kufunga kutokana na mbanano hadi kwenye milango.

Nilitamani kupiga picha nyingi ila nikashindwa baada ya kuona sura za watu zikiwa hazina matumaini, nikaona isiwe tabu ngoja nishudie kwa macho zaidi.

Wiki moja iliyopita viongozi wa Mkoa wa Dar na Wakala ya Mabasi Yaendayo Haraka (DART), Wakala ya Barabara Tanzania (TANROADS) walinukuliwa wakisema wanashughulikia changamoto hiyo ya uhaba wa magari ili isijirudie.
 
Maboresho yanayotakiwa kufanyika katika mradi wa mabasi yaendayo haraka Bus rapid transit (BRT) jijini Dar es Salaam.


Nimebaini changamoto kadhaa zinazotakiwa kutatuliwa katika mradi huu.


Hivyo nimemshauri juu ya maboresho yanayotakiwa kufanywa katika mradi huu. Pitia katika link hii kusoma ushauri wote: Kwako Mkurugenzi mpya wa Wakala wa Mabasi Yaendayo Haraka (DART): Katatue changamoto zifuatazo….


Pia michango mbalimbali imetolewa na wadau wengine na wameshauri jinsi ambavyo mfumo wa uendeshaji wa haya mabasi unapaswa kuwa ili kwendana na ukuaji wa teknolojia:


Ushauri wote tumeuandika hapa: Kwako Mkurugenzi mpya wa Wakala wa Mabasi Yaendayo Haraka (DART): Katatue changamoto zifuatazo….
 
Back
Top Bottom