BigTall
JF-Expert Member
- Mar 9, 2022
- 525
- 1,257
Jumamosi ya tarehe 30 Aprili 2022 kwenye uwanja wa Benjamini Mkapa kutakuwa na mpambano wa soka wa watani wa jadi baina ya klabu ya Simba na Yanga za Dar es salaam utakaochezwa saa 11 :00 jioni.
Katika kuelekea mchezo huo, Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam litahakikisha usalama unaimarishwa kwa kiwango cha juu.
Tuwatoe hofu mashabiki wa mpira wa miguu watakaofika kushuhudia mchezo huo kuwa ulinzi ndani na nje ya uwanja utakuwa umeimarishwa.
Jeshi la Polisi Kanda maalum ya Dar es salaam linatoa onyo kali na tahadhari katika kipindi hiki kuwa mtu yeyote atakayebainika kujihusisha na vitendo vya kihalifu ndani na nje ya uwanja atashughulikiwa kwa mujibu wa sheria.
Muliro J. MULIRO – ACP
KAMANDA WA POLISI KANDA MAALUM
DAR ES SALAM.