MSAGA SUMU
JF-Expert Member
- May 25, 2015
- 6,661
- 21,656
Nawakilisha taarifa hii hapa ili jukwaa la Kenya baada ya mtu mmoja kusema umeme Tanzania umesambaa kwa 17%.
Mwaka 2018/19 Tanzania inaingia phase ya mwisho usambazaji umeme kwa hiyo by 2022/23 Tanzania itakuwa 100% electrified.
Soma hapa.
• Kusambaza umeme kwenye vijiji 3,559 katika mikoa 25 ya Tanzania Bara unaokadiriwa kugharimu Shilingi bilioni 733.98 kutoka Serikali ya Tanzania, Norway, Sweden na Benki ya Dunia. Mradi utatekelezwa kwa kipindi cha miezi 24 kuanzia mwaka wa fedha 2016/17 hadi 2017/18. Taratibu za ununuzi zinaendelea na wakandarasi wataanza kazi mwezi Machi 2017. Hadi sasa jumla ya vijiji 4,395 kati ya vijiji 12,268 ambayo ni sawa asilimia 36 vimeunganishwa na huduma ya umeme. Baada ya kukamilika kwa mradi huu, jumla ya vijiji 7,934 sawa na asilimia 65 vitakuwa vimefikiwa na umeme. Vijiji 4,334 vinavyosalia vitapelekewa umeme kuanzia mwaka wa fedha 2018/19 hadi 2020/21 kutegemeana na upatikanaji wa fedha.
• Kusambaza umeme kwenye vijiji 121 katika maeneo yanayopitiwa na umeme wa Msongo wa Kilovoti 400 kutoka katika mikoa ya Iringa, Dodoma, Singida, Tabora na Shinyanga kwa gharama ya dola za Marekani milioni 30 kwa ufadhili wa Serikali za Norway na Sweden. Taratibu za ununuzi wa wakandarasi zinakamilishwa na utekelezaji utaanza mwezi Machi 2017.