Hali ya usambazaji umeme nchini Tanzania,Kenya mna la kujifunza Tanzania

MSAGA SUMU

JF-Expert Member
Joined
May 25, 2015
Posts
6,661
Reaction score
21,656
Nawakilisha taarifa hii hapa ili jukwaa la Kenya baada ya mtu mmoja kusema umeme Tanzania umesambaa kwa 17%.
Mwaka 2018/19 Tanzania inaingia phase ya mwisho usambazaji umeme kwa hiyo by 2022/23 Tanzania itakuwa 100% electrified.

Soma hapa.
• Kusambaza umeme kwenye vijiji 3,559 katika mikoa 25 ya Tanzania Bara unaokadiriwa kugharimu Shilingi bilioni 733.98 kutoka Serikali ya Tanzania, Norway, Sweden na Benki ya Dunia. Mradi utatekelezwa kwa kipindi cha miezi 24 kuanzia mwaka wa fedha 2016/17 hadi 2017/18. Taratibu za ununuzi zinaendelea na wakandarasi wataanza kazi mwezi Machi 2017. Hadi sasa jumla ya vijiji 4,395 kati ya vijiji 12,268 ambayo ni sawa asilimia 36 vimeunganishwa na huduma ya umeme. Baada ya kukamilika kwa mradi huu, jumla ya vijiji 7,934 sawa na asilimia 65 vitakuwa vimefikiwa na umeme. Vijiji 4,334 vinavyosalia vitapelekewa umeme kuanzia mwaka wa fedha 2018/19 hadi 2020/21 kutegemeana na upatikanaji wa fedha.

• Kusambaza umeme kwenye vijiji 121 katika maeneo yanayopitiwa na umeme wa Msongo wa Kilovoti 400 kutoka katika mikoa ya Iringa, Dodoma, Singida, Tabora na Shinyanga kwa gharama ya dola za Marekani milioni 30 kwa ufadhili wa Serikali za Norway na Sweden. Taratibu za ununuzi wa wakandarasi zinakamilishwa na utekelezaji utaanza mwezi Machi 2017.
 
Kweli kabisa tuna cha kujifunza kutoka kwa Watanzania. Ukipita pale Kariakoo unachoshwa na makelele
na mimoshi mingi. Ukiingia kwenye maduka ni giza tu. Yeah, tutajifunza kutoka kwenu.
Utachoka jombaa, yaani hata kula chipsi mayai tu, juhudi za kulenga shabaha kwenye midomo ndo shughuli yote! 😉
 
Kwenye 'connectivity' yaani usambazaji wa umeme, Kenya tulishafikia 67%, wengine hapa wanalala kwa 'lullaby' za migurumo ya majenereta! Tuna nini cha kujifunza kutoka Tz? Nini?
Habari za kweli hizi?
 
Kwenye 'connectivity' yaani usambazaji wa umeme, Kenya tulishafikia 67%, wengine hapa wanalala kwa 'lullaby' za migurumo ya majenereta! Tuna nini cha kujifunza kutoka Tz? Nini?
Weka ushahidi wacha longolongo, Kenya mpo 63% Tanzania is 68%, lete ushahidi acha domo tupu. Katika huduma zote muhimu za kijamii kama umeme connectivity, water, heath, roads and employment, Kenya imeachwa mbali sana na Tanzania, tafadhali lete ushahidi wenye taarifa za karibuni uone mambo yalivyo.
 
Watanzania huwa mnatia huruma, liinchi lote hilo giza na mna kila aina raslimali za kuweza kusambaza umeme kwa kila nyumba.
2025 ndio mnategemea kufikia asilimia 50% ya usambazaji wa umeme Rural Electrification - TanzaniaInvest
Sisi sasa hivi tunachezea kwenye 70%, tulikua 60% mwaka wa 2016 kumekua na massive connectivity imekua ikiendelea.
Mpo mbali sana kuwaza ushindani na Kenya, mtafute viinchi kama Malawi ligi zenu huko SADC.
 
Leta source hapa toune takwimu
 
Mara ya mwisho umrpita kkoo lini?
Kweli kabisa tuna cha kujifunza kutoka kwa Watanzania. Ukipita pale Kariakoo unachoshwa na makelele
na mimoshi mingi. Ukiingia kwenye maduka ni giza tu. Yeah, tutajifunza kutoka kwenu.
M
 
Kwenye 'connectivity' yaani usambazaji wa umeme, Kenya tulishafikia 67%, wengine hapa wanalala kwa 'lullaby' za migurumo ya majenereta! Tuna nini cha kujifunza kutoka Tz? Nini?
Leta chanzo cha hiyo habari tusome
 
Weka ushahidi wacha longolongo, Kenya mpo 63% Tanzania is 68%, lete ushahidi acha domo tupu. Katika huduma zote muhimu za kijamii kama umeme connectivity, water, heath, roads and employment, Kenya imeachwa mbali sana na Tanzania, tafadhali lete ushahidi wenye taarifa za karibuni uone mambo yalivyo.
Ulivyo muongo unafaa uaibike....by the end of 2016 data from world bank ilkua inaonesha electricity access rate Kenya ilkua 60% na Tanzania 36%..haiezi kuwa in one year mmetoka from 36% to 68% na kuipiku kenya
East Africa on track to boost energy access, says World Bank
 
Back
Top Bottom