Halima Mdee amcharukia Kimei Bungeni, kuhusu deni la Serikali kwa mifuko ya hifadhi ya Jamii

Halima Mdee amcharukia Kimei Bungeni, kuhusu deni la Serikali kwa mifuko ya hifadhi ya Jamii

Mbunge Halima Mdee amemcharukia Mbunge wa Vunjo Charles Kimei baada ya Halima Mdee kuchangia kuwa Serikali imekopa fedha nyingi kwenye mifuko ya hifadhi za jamii kiasi cha trilioni 10 na kufanya mifuko hiyo na kutolipa madeni hayo kumefanya mifuko hiyo kushindwa kulipa mafao ya wastaafu ipasavyo.

Kimei aliingilia kati na kusema kuwa deni hilo haliathiri mifuko ya jamii kulipa mafao kwani mifuko hiyo pia ni sehemu ya serikali na serikali inaweza kuwapa fedha hizo wakati wowote endapo watakwama ndipo Halima Mdee akamcharukia.

Zaidi waweza kuwaikiliza mwenyewe.


Halima alishachafua legacy yake hana jipya huyo! Amebaki kuongea kwa sauti tu kama kiziwi!
 
Ndiyo maana wasomi wanaenda kwenye kupiga nyungu badala ya kutengeneza exportable chanjo(vaccine) ya Coronavirus! Nyungu ileile ya mababu zetu wa miaka ya Nabii Musa!!! Kama wangaliweza kuuza hiyo njungu Uchina, India, Russia Uingereza hapo ingejulika umuhimu wa wasomi wetu!!
Kwani lengo la tiba ni nini?
Hivi mtu akitumia njia anazozijua yeye na akapata nafuu kama si kupona kuna shida gani? Au kwako wewe tiba ni lazima iwe chanjo?
 
Mzee Kimei anajidhalilisha bure. Badala ya kuwatetea wananchi waliompeleka bungeni ili awawakilishe, anaitetea serikali utadhani ni waziri.
Lakini pia anatoa majibu ambayo hayalengi tatizo la msingi analozungumzia mh. Halima Mdee.
Hoja ya msingi ni kwamba, wastaafu hawalipwi mafao yao kwa kuwa mifuko ya hifadhi ya jamii haina fedha kwa sababu pesa zao (zaidi ya trillion10) zilikopwa na serikali. Mh. Mdee kaomba serikali itenge angalau sh. Trillion 1 kila mwaka ikiwa ni marejesho ya deni kwenye mifuko hiyo.
Mzee Kimei kumbuka hukwenda bungeni kuitetea serikali bali kuwatetea wananchi wanyonge waliokuchagua.
 
Kimei kama nawe umeuza akili zako kwa ajili ya kusaka uwaziri utakuwa umeuza kabisa utu wako. Shame!
 
Dhamana hailipi deni, Kimei inatakiwa arudi shule, 'Kimei is running out of ideas, he has to go back to school, Assets do not pay loans' defending for the sake of defending, is convincing those who do not know it. ndiyo maana Msukuma watu wanampa hekoo! kwakuwashangaa wasomi wanao jito ufahamu, hapo awali nilidhani anafaa kuwa waziri wa fedha kumbe nilikosea
Mimi nilishaona huyu jamaa Hafai kupewa uongozi mkubwa
 
Back
Top Bottom