Halima Mdee amcharukia Kimei Bungeni, kuhusu deni la Serikali kwa mifuko ya hifadhi ya Jamii

Halima alishachafua legacy yake hana jipya huyo! Amebaki kuongea kwa sauti tu kama kiziwi!
 
Kwani lengo la tiba ni nini?
Hivi mtu akitumia njia anazozijua yeye na akapata nafuu kama si kupona kuna shida gani? Au kwako wewe tiba ni lazima iwe chanjo?
 
Mzee Kimei anajidhalilisha bure. Badala ya kuwatetea wananchi waliompeleka bungeni ili awawakilishe, anaitetea serikali utadhani ni waziri.
Lakini pia anatoa majibu ambayo hayalengi tatizo la msingi analozungumzia mh. Halima Mdee.
Hoja ya msingi ni kwamba, wastaafu hawalipwi mafao yao kwa kuwa mifuko ya hifadhi ya jamii haina fedha kwa sababu pesa zao (zaidi ya trillion10) zilikopwa na serikali. Mh. Mdee kaomba serikali itenge angalau sh. Trillion 1 kila mwaka ikiwa ni marejesho ya deni kwenye mifuko hiyo.
Mzee Kimei kumbuka hukwenda bungeni kuitetea serikali bali kuwatetea wananchi wanyonge waliokuchagua.
 
Kimei kama nawe umeuza akili zako kwa ajili ya kusaka uwaziri utakuwa umeuza kabisa utu wako. Shame!
 
Mimi nilishaona huyu jamaa Hafai kupewa uongozi mkubwa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…