Halima Mdee, Dorothy Semu, na Dkt. Dorothy Gwajima ni baadhi ya mifano Bora ya Wanawake kwenye Siasa na Uongozi

Halima Mdee, Dorothy Semu, na Dkt. Dorothy Gwajima ni baadhi ya mifano Bora ya Wanawake kwenye Siasa na Uongozi

Lady Whistledown

JF-Expert Member
Joined
Aug 2, 2021
Posts
1,147
Reaction score
2,008
Halima Mdee

Alikuwa Mbunge wa Kawe kuanzia 2010 hadi 2020 (CHADEMA) akiwa miongoni mwa Wanawake wachache walioweza kuingia Bungeni kwa kupitia vyama vya Upinzani. Aliwahi pia kuwa mwenyekiti wa BAWACHA

Dorothy Semu

Mwaka 2020 aliteuliwa kuwa Makamu Mwenyekiti Bara na Chama cha ACT-Wazalendo, huku Machi 2024 akichaguliwa kuwa Kiongozi wa Chama hicho

Dkt. Dorothy Gwajima

Mwaka 2020 aliteuliwa kuwa Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto. Dkt. Gwajima amekuwa mstari wa mbele katika masuala ya Kijinsia na afya, hasa akisisitiza Usawa na nafasi za Wanawake katika jamii

Tunapowatazama Wanawake kama Halima Mdee, Dorothy Semu, na Dkt. Dorothy Gwajima, tunapata nguvu na msukumo mpya wa kushiriki katika siasa na nafasi za uongozi.

Kwa ujasiri na uvumilivu wao, wameweza kuvunja mipaka, kushinda changamoto, na kuwa sauti ya mabadiliko ndani ya jamii zetu.

Halima alionesha ujasiri wa kupaza sauti ya wanyonge, Dorothy aliongoza kwa kuweka wanawake na vijana mstari wa mbele, na Dkt. Gwajima alitoa mchango mkubwa katika sekta ya afya kwa maslahi ya wananchi.

Wanawake hawa ni ushahidi kuwa hakuna lisilowezekana kwa mwanamke anayeamini katika uwezo wake. Tunapoyaona mafanikio yao, tunahamasika kujiamini, kujiunga katika mijadala ya kisiasa, na kutumia sauti zetu kuleta mabadiliko tunayoyataka.

Hivyo basi, kwa wanawake na wasichana wa Tanzania, simama na uamini kuwa unao uwezo wa kuleta mabadiliko - jiunge katika siasa na simama kama sauti ya mabadiliko katika taifa letu
 
Halima covid 19 scandal imeharibu CV yake aliyoijenga tangia 2004....Lakini simlaumu maana adui muombee njaa atanyoosha mikono juu hata kama alikuwa shujaa.
 
Back
Top Bottom