Halima Mdee: Mimi pamoja na timu yangu (Wabunge 19) tutabaki kuwa WanaCHADEMA kindakindaki. Tutaenda kuyajenga ndani kwetu

Halima Mdee: Mimi pamoja na timu yangu (Wabunge 19) tutabaki kuwa WanaCHADEMA kindakindaki. Tutaenda kuyajenga ndani kwetu

Replica

JF-Expert Member
Joined
Aug 28, 2017
Posts
1,681
Reaction score
8,887
Wabunge 19 viti maalum kupitia CHADEMA ambao waliapishwa na Spika Ndugai kisha kufutiwa uanachama na chama chao leo wanaongea na waandishi wa habari. Tayari wabunge hao wanawake wamefika ukumbi wa Regency wakiwa wamevalia sare za CHADEMA almaarufu 'Gwanda'. Kuwa nami kukujuza watachokiongea.


19.jpg

=========

9:32 Asubuhi: Halima Mdee na Ester Bulaya kufika baada ya dakika kumi kutokana na kuchelewa

9:45 Asubuhi: Halima Mdee na Ester Bulaya wameingia ukumbini na kinachoendelea ni burudani ya wimbo wa Halima Mdee

9:48 Asubuhi: Ester Lambert anafanya utangulizi na kumkaribisha mzungumzaji, Halima Mdee

Halima Mdee: Niombe radhi kwa kuchelewa dakika 15 kwani ilikuwa tuanze saa tatu na nusu, pili nitambue uwepo wa wazazi wangu wapo na mimi siku zote kwa shida na raha. Tatu nitambue uwepo wa viongozi wenzangu, hawa ni timu ya BAWACHA ambalo tumelizalisha baada ya kazi nzuri sana tuliofanya kujenga baraza nikiwa na timu yangu.

Vile vile tuna viongozi wa chama wanawake na wa kanda pia tuna katibu mkuu wa BAVICHA, Nusrat Hanje mstaafu vilevile tuna wabunge wa Bunge lililopita.

Nimekuja leo kuzungumza na nyie kwa sababu moja kubwa, niliamua kukaa kimya lakini ukikaa kimya vilevile unawapa nafasi wengine wanaongea, wanatengeneza uongo mwingi na uongo ukiwa mwingi unaonekana ni ukweli, imenilazima nije nizungumze kwa nia ya kutuliza haya mambo kwa sababu sio makubwa kama ambavyo yanataka yawe.

Mimi ni mwanachadema na nimekuwa mwanachadema kwa miaka 16 na kwangu mimi ukiacha wazazi wangu, familia yangu ya pili ni CHADEMA na katika muktadha huo maana kuna watu wanasema anakuja kuunga juhudi sijui, pamoja na kwamba mimi na wenzangu tumechukuliwa hatua za kinidhamu na viongozi wetu kwa mantiki ya kamati kuu, niwahakikishie mimi pamoja na timu yangu tutabaki kuwa wanachadema kindakindaki, nataka hilo niliweke wazi.

Mimi sina dhamira ya kuondoka CHADEMA, wenzangu, unaambiwa usiseme nafsi ya mtu lakini kwa historia yao ndani ya chama, hapa sihani kama kuna mtu ana pungufu ya miaka 5 ndani ya chama, kuna miaka 5, wengine wana miaka 10, wengine tuna miaka 16, wengine wana miaka 30 kwahiyo kila mmoja hapa ameijenga CHADEMA, amesaidia kuijenga CHADEMA kwa jasho na damu yake.

Pamoja na changamoto ambayo tunapitia, niwahakikishie wanachadema nchi nzima, Halima mnaemfahamu miaka yote ndio halima yuleyule na uaminifu wake kwa chama utabaki vilevile na ninaamini nikisema Halima maana yake na timu yangu.

Kumekuwa na maneno mengi, kuna watu wanasema Halima amenunuliwa, amepata mpunga mrefu, niseme hivi, mimi Halima Mdee sijawahi kununuliwa, sitanunuliwa, sitarajii kununuliwa.

Watu waliofanya kazi na mimi iwe kwenye chama, bungeni wanajua ukiambiwa taja watu watatu ambao rushwa kwao ni mwiko inawezekana Halima nikawa namba moja. Kwa hiyo mimi sina thamani ya kipande cha fedha, kazi zangu zote nimekuwa nikifanya kwa uaminifu na kwa mapenzi kutoka moyoni, sina maigizo.

Maana sasa hivi wanasema Mdee na wenzake maana mimi ndio napigwa mawe kwelikweli, fedha ukipewa haina siri, yani kama nimepewa bilioni 1, kama milioni 200 haina siri, ama itakuwa kwenye akauti ama itakuwa nyumbani kwenye sandarusi.

Kwakuwa haina siri walionipa watasema kama hapa ninawakana kama hawajanipa, wanasema Halima tulikupa tarehe fulani, hakuna yeyote aliepewa hela na kama kuna mambo yoyote yaliyotokea yalikuwa na dhamira nzuri kabisa ya kujenga taasisi imara, kustreghthen baraza la wanawake.

Hakuna alielipwa, mimi ni muhanga wa siasa za nchi hii, muhanga kwelikweli na tunavyozungumza kuna makesi mengine yaliyobaki. Tunavyozungumza juzi tumetoka kwenye uchaguzi mkuu, mimi kati ya wagombea wengi, ni bahati mbaya mainternet yalizimwa, mimi kati ya wagombea wengi ndiyo nilikuwa wa kwanza kwenda kwenye vituo asubuhi kuonyesha namna uchaguzi umekuwa rigged kwa hiyo nitakuwa mwendawazimu, jana nimeonyesha uchaguzi ulivyoenda halafu leo ninapokea mpunga, so what.

Kila mtu ametoka kwake hapa, hatujawahi kupata ulinzi sio tu wa usalama wa Taifa hata wa mgambo. Hakuna ulinzi wowote, sisi tulindwa na Mungu kwa hiyo ninashauri sana huyo mtu huko ajue kwamba atasubiri sana kama ataweza akanchonganisha na chama changu, atasubiri sana kama anadhani anaweza akanichonganisha na wanachama na Taifa kwa ujumla.

USULI WA MAMBO
Halima Mdee:
Kuhudhuria kamati kuu, tarehe 25 mimi binafsi nilipata barua saa kumi kasorobo jioni, nilipata barua kwa njia ya simu naamini mheshimiwa Matiko naye hakupata lakini wengine kila mtu alipata kwa muda wake yeye lakini wote kwa wote tulipata tarehe 25 tukitakiwa kuhudhuria kikao cha kamati kuu tarehe 27 saa mbili asubuhi.

Kutokana na sintofahamu iliyojitokeza, tarehe 26/11 tulimuandikia barua katibu mkuu tukimuomba asogeze kikao mbele japo kwa wiki moja na tulifanya hivyo, mosi utaratibu wetu wa katiba wa kikawaida, unasema mtu anatakiwa kujulishwa makosa yake kwa maandishi na kutakiwa kutoa majibu katika muda usiopungua wiki mbili apewe nafasi ya kujitetea mbele ya kikao kinachohusika na baada ya kusikilizwa na kujitetea, uamuzi utatoka baada ya wiki mbili lakini katiba yetu vilevile inaruhusu mazingira ya dharura ambayo kama tunadhani kwa maslahi ya chama jambo linahitaji kusikilizwa haraka, linaweza likasikilizwa kwa haraka.

Siko hapa kusema kwamba, tulivyopewa short notice kulikuwa na makosa, hapana. Short notice ilikuwa ni sahihi kwa mtu alieandika barua ya suala la dharura lakini kwa upande wetu tulidhani kutokana na presha kubwa iliyopo na kutokana na press ambayo ilikuwa imeshazungumzwa na katibu mkuu ikaongea mambo mazito sana, tukadhani ni busara labda tuombe extension ili hasira zetu zipungue, kila upande ulikuw na haki ya kuwa na hasira vile ilivyokuwa kwa hiyyo tuliandika barua ya kuomba extension ya wiki moja tukitambua kwamba katiba ina provision inayosema si chini wiki mbili ili ituwezeshe kila mmoja wetu tukiweza kwenda kwenye kikao, twende kwenye kikao hasira zikiwa zimepungua kidogo ili tukifanya maamuzi, tusifanye maamuzi yenye hasira kali.

=>Ijumaa tarehe 27 tulivuliwa uanachama na nyadhifa zote. Hapa tumevaa kombati, sisi tutaendelea kuwa wanachama wa hiyari ndani ya CHADEMA

=> Tutafanya michakato ya kikatiba ndani ya chama, jana jioni Mimi nilipata barua kutoka kwa Katibu Mkuu ya taarifa ya uamuzi

=>Muda ambao tulitakiwa kufike kwenye kikao kulikuwa na uhamasishaji kwenye Mitandao ya Kijamii wa baadhi ya viongozi wakihamasisha watu waje watupige mawe, watupige mayai viza

=> Tulidhani kiusalama haikuwa jambo rahisi kuhudhuria kikao katika mazingira hayo

=>Tutaanza kutafakari pamoja na wanasheria wetu ili kuangalia ni namna gani bora tunaweza kutatua tatizo hili

=> Leo sitaki kuwa na story nyingi, itoshe kusema tunaipenda CHADEMA ana hatutaondoka CHADEMA tutabaki wanachama wa hiari mpaka pale tutakapenda kujadili

=>Mwenyekiti (Freeman Mbowe) alisema hawa wanawake 19 ni majembe kweli kweli. Mimi kupoteza jeshi kama hili ni jambo ambalo sitalipenda

=> Tutaenda kuyajenga ndani kwetu, leo sitaki kuongea mambo mengi kwasababu ninyi wanahabari mnatafuta habari

=>Nataka hili jambo tulimalize, lirudi kwenye channel za chama. Sio sawa chama chetu kuwa kwenye magazeti, huyu anaongea hili na mwingine anaongea lile

=> Mliofuatilia mlishuhudia siku ya kikao kuna watu walijitokeza lakini si kwa kiwango kilichohamasishwa

=>Katika chaguzi zote tangu vyama vingi vimeanza kuanzia 2010, 2015 na 2020 hakuna uchaguzi ambao tuliuukubali

=>Lakini Wabunge si walienda? Kwanini 2020 wasiende mpaka sasa Madiwani wanaapa na Mbunge aliyechaguliwa ameapa
Usishangae sisi au wengine wakienda

=>Kutokubali Uchaguzi haimaanishi hautaingia kwenye vikao vya maamuzi kwa ngazi ya nchi. Mimi sidhani kama ni ujanja kukimbia kwenye vyombo vinavyofanya maamuzi

=>Unasema mapungufu kisha unaenda kwenye vikao hivyo kupambana na changamoto hiyo
 
Wabunge 19 viti maalum kupitia CHADEMA ambao waliapishwa na Spika Ndugai kisha kufutiwa uanachama leo wanaongea na waandishi wa habari. Tayari wanawake hao wameshafika ukumbini wakiwa wamevalia sare za Chadema almaarufu 'Gwanda'. Kuwa nami kukujuza watachokiongea.
Picha tafadhali
 
Natarajia kuwa watakubaliana na uamuzi wa CHADEMA

Kutokutii hayo ni kujiporomosha kisiasa na ni kushindana na taasisi ambayo huto weza kushinda kamwe na ukishinda ni kwa figisu ambazo hazito kusaidia maana una someka sio mwenzao.

Pia nategemea nitasikia wakisema tuna jiuzuru nyazifa za ubunge viti maalum kwa kuwa tulifikiri tofauti na kuzani zina baraka ya chama kumbe hapana.

Mambo rahisi sana nashangaa wana jitutumua pasina msingi wowote.

NB:
Chukueni mfano wa Mh. Mwanadiplomasia nguli B. Membe alishindana na chama lakini hakushinda, aliishia kukubaliana na maanlmuzi ya chama na kukaaa pembeni
 
Back
Top Bottom