Halima Mdee: Mimi pamoja na timu yangu (Wabunge 19) tutabaki kuwa WanaCHADEMA kindakindaki. Tutaenda kuyajenga ndani kwetu

Halima Mdee: Mimi pamoja na timu yangu (Wabunge 19) tutabaki kuwa WanaCHADEMA kindakindaki. Tutaenda kuyajenga ndani kwetu

Ukweli ulikuwa upi zaidi ya kushawishiwa na CCM na kuwarubuni..... hawa wadada wakajisahau namna walivyokuwa wanavurumishwa na hao hao ambao leo wamewakumbatia.
Hivi inawezekana kwa mtu mzima mwenye akili zake timamu mwanachama kindakindaki akashawishiwa kirahisirahisi hivyo. Wewe unaweza kushawishiwa kwa namna hiyo.
 
Tunawasubiri kwa ham watupe ukweli wa manyanyaso ndani ya chadema, kuna watu wametendewa mabaya sn ndani ya chadema
Pia ccm imewatendea watz unyama wa kishetani... Yupo wapi ben saa8, mawazo, azory, diwan kilombero, katibu ananasifu? Kwenu kuua na kutesa n km dua na sio manyanyaso!
 
Hao waliochelewa watakuwa walienda Lumumba kupokea maelekezo ya mwisho juu ya nini wakaongee na wanahabari, hao wanawake ni weupe sana vichwani, wamekosa "organisation" kabisa juu ya hili suala lao.

Sasa wanaendelea kutetewa na Ndugai ndio wanazidi kuonekana vituko.
 
Wabunge 19 viti maalum kupitia CHADEMA ambao waliapishwa na Spika Ndugai kisha kufutiwa uanachama na chama chao leo wanaongea na waandishi wa habari. Tayari wabunge hao wanawake wamefika ukumbi wa Regency wakiwa wamevalia sare za CHADEMA almaarufu 'Gwanda'. Kuwa nami kukujuza watachokiongea.

=========

9:32 Asubuhi: Halima Mdee na Ester Bulaya kufika baada ya dakika kumi kutokana na kuchelewa
Hakika binadamu hubadilika!

Heri hata ya fisi.
 
Naona wameingia na Magwanda yao .... next step ni kukata rufaa ndani ya chama ili kuchelewesha mambo!!

Baada ya vikao vya ndani watakwenda mahakamani.
 
Hii vita nilishasema, Halima na wenzake walishashinda, bado wana move nyingine kama mbili hivi mbele yao wakati CHADEMA wamefikia ukomo.

Hawa ni wabunge wa CHADEMA hadi 2025 kwa vyovyote na wataendelea kuwa wanachama halali kupitia mahakama.
 
Natarajia kuwa watakubaliana na uamuzi wa CDM

Kuto kutii hayo ni kujipolomosha kisiasa na ni kushindana na taasisi ambayo huto weza kushinda kamwe na ukishinda ni kwa figisu ambazo hazito kusaidia maana una someka sio mwenzao...

Pia nategemea nitasikia wakisema tuna jiuzuru nyazifa za ubunge viti maalum kwa kuwa tulifikiri tofauti na kuzani zina baraka ya chama kumbe hapana...

Mambo rahisi sana nashangaa wana jitutumua pasina msingi wowote

NB:
Chukueni mfano wa Mh. Mwanadiplomasia nguli B. Membe alishindana na chama lakini hakushinda, aliishia kukubaliana na maanlmuzi ya chama na kukaaa pembeni
Chezea pesa siyo ajira!
Miaka 5 mbunge, na kuinua mgongo cha kustaafu kinono!
Nyie endeleeni kura vumbi hapo ufipa
 
Wabunge 19 viti maalum kupitia CHADEMA ambao waliapishwa na Spika Ndugai kisha kufutiwa uanachama na chama chao leo wanaongea na waandishi wa habari. Tayari wabunge hao wanawake wamefika ukumbi wa Regency wakiwa wamevalia sare za CHADEMA almaarufu 'Gwanda'. Kuwa nami kukujuza watachokiongea.

=========

9:32 Asubuhi: Halima Mdee na Ester Bulaya kufika baada ya dakika kumi kutokana na kuchelewa

9:45 Asubuhi: Halima Mdee na Ester Bulaya wameingia ukumbini
Picha inajieleza zaidi nadhani kuliko watakayoongea!
 
Back
Top Bottom