Halima na wenzake licha ya kukosa majibu ya msingi mfano ilikuwaje wajipeleke kuapishwa ikiwa chama hakikuwa kimefanya uteuzi wa wabunge; saini ya katibu mkuu wa chama waliipate wakati KM mwenyewe alisema wazi hajapeleka majina; kwa nini walikiuka utaratibu wa chama n.k lakini pia wamejaribu kuleta hoja ya kwamba mwaka 2010 na 2015 chama kiligomea matokeo lakini bado walienda bungeni.
Ni hoja dhaifu tu. Kwa sababu mwaka 2010 na 2015 chama kiligomea na kutotambua matokeo ya Urais pekee. Ndio sababu walitoka nje alipoalikwa kuhutubia bunge. Walitoka sababu hawakuwa wanatambua matokeo yaliyompa ushindi. Safari hii, 2020 chama kimegomea matokeo yote ya uchaguzi mkuu.
Hakiyatambui na msimamo wa chama ni uchaguzi kurudiwa upya chini ya tume huru ya uchaguzi (kama ilivyotokea Malawi). Hivyo chama hakitambui chochote kilichotokana na uchaguzi (ikiwamo hizo asilimia za ubunge wa viti maalum) kwa sababu walikamata kura fake za udiwani, ubunge na urais, mawakala waliondoshwa kabla/wakati wa kupiga kura na/au kuhesabu kura n.k. Hivyo, msimamo wa chama ni kutotambua matokeo yote ya uchaguzi na kutaka urudiwe.
Halima na wenzake wamekamatwa pabaya. Wamefutwa uanachama sharti waamue mambo mawili tu: Kukiri, Kujutia, na kuomba msamaha CHADEMA na kuukana ubunge wao, au kuhamia ccm moja kwa moja na kuendelea na mambo mengine.
Kwa upande wa CHADEMA, wao wameongeza credibility yao kwa wananchi kwa kuonesha kivitendo kwamba kipaumbele si fedha za ruzuku ama ubunge bali uhuru, haki, na maendeleo ya watu kama kauli mbiu yao ya uchaguzi ilivyoainisha. Hivyo katika mchezo huu CHADEMA ameshinda points, sirikali hasa kwa ile movie ya Nusrat IMEPOTEZA BIG TIME, Halima & co. wamepoteza in the long term.