Halima Mdee na wenzake 18 wagoma kufika Kamati Kuu ya chama kwa madai ya kupokea vitisho toka kwa viongozi na wanachama wa CHADEMA

Halima Mdee na wenzake 18 wagoma kufika Kamati Kuu ya chama kwa madai ya kupokea vitisho toka kwa viongozi na wanachama wa CHADEMA

Muda mfupi kabla Kamati kuu CHADEMA kuwahoji wanachama wake walioapishwa kuwa wabunge wa viti maalum, wanachama hao wamesisitiza kutotokea mbele ya kamati kuu wakidai kupokea vitisho toka kwa viongozi na wanachama wa CHADEMA wakihofia usalama endapo watafika ofisi za chama hicho.

--
Awali Baraza la Wanawake wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (BAWACHA) leo waliandamana katika ofisi za makao makuu ya chama hicho zilizopo Kinondoni Dar es Salaam, kushinikiza kutowahitaji wabunge Halima Mdee, Ester Bulaya na wengine walioapishwa viti maalum.
COVID 19 ilishafukuzwa na rais John Pombe Joseph Magufuli tangu March 2020
Halima na wenzie 18 watamalizana bungeni hawataki maneno
 
Mkuu Mbowe mjanja sana!

Kawaambia wasiende ili ionekane hawajafukuzwa kwakuwa hawakufika kwenye kamati kuu
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
Michezo hii kina salary slip hawawezi kuielewa.
Mnaishi kwa propaganda za kipuuzi!
 
Mkuu huu mchezo utaisha hivihivi kihuni, kitendo cha kutosoma,kusikia wala kumuona Mbowe popote kwenye hii ishu ya akina Mdee ni picha tosha ya kinachoendelea. Tatizo wafuasi wengi wa CHADEMA ni kama mna amini CHADEMA ilikuwa inapigania maslahi ya wananchi. Hapo ndo mlipokosea, Ila Mungu si Athumani hii ishu itawafumbua macho. Kama ya kubadili gia angani ya Lowassa haikuwafumbua macho.
Mkuu tusiandikie mate, acha tuone hitimisho. Kama ni kupigania wananchi tuliona kwa macho yetu na wala usitake kupotosha kwa hii hali ya hawa wahuni wachache. Ni mangapi yamefanyika kwa msukumo wa hao cdm tunawajua, sasa unapokuja na lugha za jumla sijui unaona unaoongea na mtoto?
 
Mnaishi kwa propaganda za kipuuzi!
Ndio maisha yetu haya.
EmnTYwKXUAErZPf.jpg
 
COVID 19 ilishafukuzwa na rais John Pombe Joseph Magufuli tangu March 2020
Halima na wenzie 18 watamalizana bungeni hawataki maneno

Mwambie atumie nguvu hizo hizo kufukuza ukimwi.
 
Sijui kwanini chadema wa mitandaoni ni wajinga sana kugundua hii janja ya akina Mbowe kama hakuna kamati imekutana leo
 
Viongozi gani na wamesema wanachofanya kina Baraka za mwenyekiti?
 
Trillion mbili za mabeberu zinawatoa jasho CCM kutaka kuunda Kambi rasmi Bungeni kwa nguvu.

Habari mbaya ni kwamba wote 19 wanajivua ubunge wa Ndugai rasmi leo.

Stay turned!!
Wenzio wameshajaza na fomu za mkopo hivyo.

Kama mijanaume mizima ilinunuliwa kama njugu ndio sembuse hawa mademu unaoweza kuwalaghai hata bila ya pesa?
 
Muda mfupi kabla Kamati kuu CHADEMA kuwahoji wanachama wake walioapishwa kuwa wabunge wa viti maalum, wanachama hao wamesisitiza kutotokea mbele ya kamati kuu wakidai kupokea vitisho toka kwa viongozi na wanachama wa CHADEMA wakihofia usalama endapo watafika ofisi za chama hicho.

--
Awali Baraza la Wanawake wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (BAWACHA) leo waliandamana katika ofisi za makao makuu ya chama hicho zilizopo Kinondoni Dar es Salaam, kushinikiza kutowahitaji wabunge Halima Mdee, Ester Bulaya na wengine walioapishwa viti maalum.
Kama wanawaogopa wanachama wenzao inamaana wamejitoa uanachama wa Chadema na kuanzisha kikundi chao, basi CC iwafute kwa kujitoa wenyewe.
 
Back
Top Bottom