Halima Mdee na wenzake 18 wagoma kufika Kamati Kuu ya chama kwa madai ya kupokea vitisho toka kwa viongozi na wanachama wa CHADEMA

Halima Mdee na wenzake 18 wagoma kufika Kamati Kuu ya chama kwa madai ya kupokea vitisho toka kwa viongozi na wanachama wa CHADEMA

Naona mnaitafuta damu ya waTanzania kwa kila njia iwezekanayo, je, mtaimwaga kweli?

Inawaumiza sana kutopata watu wa kuwaua?
Kumbe unaogopa kuuliwa basi kaa utulie sio unaanza kuwaita watu wasaliti watu ambao hawakuogopa kuuliwa katika harakati za kudai haki walizidai hadharani tofauti na wewe uliyejificha humu JF unaogopa hata kuandamana,si ajabu nawe unakula keki ya taifa vizuri tu ila humu mnakuja kuleta unafki na ndio maana hamuwezi kuandamana kudai haki mnajificha.
 
mbowe aseme ukweli asitake kuremba maneno kwa aiji ya kuutetea uenyekiti wake. la sivyo ajibu maneno/tuhuma aliyo yatamka mdee mara baada ya kula kiapo, mdee sio mjinga amsingizie Mbowe.
yaani kweli watu wote tunaonekana hatuwezi kufikiria kisa kumlinda mtu mmoja?! kwani huwezi kuachia nafasi kwa heshima tu kuliko kuumbuka ?!
mambo yamevurugika na wewe ndio kiongozi step down kwa heshima pisha wengine warudishe heshima ya chama na imani ya wanachama
Hivi wewe TAGA, umejiunga lini CHADEMA?
 
yaani hapa tuanze na Mwenyekiti mwenyewe, aulizwe iweje Mwenyekiti wa Bavicha adiriki kutamka kuwa yeye Mbowe karidhia mchakato? afafanue ilikuwaje mpaka mdee amsingizie maneno hayo kama kweli hakuhusika?
 
Mijitu humu yenyewe ndio wasaliti wakubwa kwakujificha humu JF wanashindwa kudai haki kwa vitendo,Mange alishaliona hilo na juzi kati Lissu nae kaliona hilo. Halafu leo unaenda kumwita Halima mdee msaliti!!!!!
 
Sasa wewe utakuwa na tofauti gani na wakina mdee kwa sababu leo hii mnawapigia kelele mdee na wenzake kwa kukiuka maamuzi ya vikao ya kutotambua matokeo ya uchaguzi wakati huohuo wewe unasahau kitendo Cha kupinga au kutokubali ujio wa wakina Lowasa wakati walipokelewa kwa maamuzi ya vikao haouni Kama wewe nawe ni walewale huna tofauti na walichokifanya wakina mdee

Kwanza jitahidi unapoandika uweke koma ama nukta, hii itasaidia kujua najadili na mtu mwenye uelewa wa kiwango gani. Ukitaka kujua tofauti ya uteuzi wa Lowassa na Lisu, angalia Lowassa alichaguliwa na kina nani kuwa mgombea wa urais, na Lisu alichaguliwa na watu gani kugombea urais. Ukimaliza hapo uje kwa mjadala, huku ukizingatia kanuni bora za uandishi.
 
Mijitu humu yenyewe ndio wasaliti wakubwa kwakujificha humu JF wanashindwa kudai haki kwa vitendo,Mange alishaliona hilo na juzi kati Lissu nae kaliona hilo. Halafu leo unaenda kumwita Halima mdee msaliti!!!!!

Mange na Lisu waliona nini tafadhali?
 
Ukiwaona machoni Ni Kama wamehamishia Tabia ya CCM kwenye meza ya pili. Ninajua CCM itawakumbatia kwa sababu wao katiba siyo kitu kwao
 
Kama Mdee, Ester(s) wameweza, je nawe 'Erythro' unaweza?

Hawa watu wamepewa nini?

Hii habari ya akina Halima Mdee, Ester Bulaya, Ester Matiko..., haya ni matokeo ya udhaifu mkubwa ndani ya chama, au ni mwendelelzo wa tabia ya unafiki tuliyonayo waTanzania?

Hakuna jambo lolote tunaloweza kulisimamia na kujitoa kwa kila kitu kulisimamia?

Wametoa maelezo yoyote kwa nini wamechukua hatua ya ajabu kiasi hiki, ya kusaliti kila kitu walichodhaniwa wanakisiamamia?
Wamelewa heshima waliyopewa ndani ya chama kwa miaka mingi , unajua ukimheshimu mtu kwa muda mrefu sana hujisahau na kudhani heshima aliyopewa alizaliwa nayo , kila mmoja wao amenunuliwa kwa hela za madafu 600mil , hii ndio hela iliyowadhalilisha na kuwaharibia katika kipindi chote walichosaliwa nacho hapa dunia , matiko , mdee na bulaya wameahidiwa unaibu Waziri , Mmoja aliyeburuzwa na anayeweza kusamehewa ni Nusrat Hanje .

Umeuliza kama mimi naweza kununuliwa hasa baada ya Mdee kujiuza , kwa kifupi nikujibu tu kwamba mimi siwezi kununuliwa kwa sababu sifanyi siasa ya kujikimu , mimi na wachache kama Mbowe tuliingia kwenye siasa tukiwa na hela nyingi kwa lengo la kusaidia utawala wa haki na demokrasia nchini Tanzania .
 
Muda mfupi kabla Kamati kuu CHADEMA kuwahoji wanachama wake walioapishwa kuwa wabunge wa viti maalum, wanachama hao wamesisitiza kutotokea mbele ya kamati kuu wakidai kupokea vitisho toka kwa viongozi na wanachama wa CHADEMA wakihofia usalama endapo watafika ofisi za chama hicho.
--
Awali Baraza la Wanawake wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (BAWACHA) leo waliandamana katika ofisi za Makao Makuu ya chama hicho zilizopo Kinondoni Dar es Salaam, kushinikiza kutowahitaji wabunge Halima Mdee, Ester Bulaya na wengine walioapishwa viti maalum.

Updates

PICHA: Wajumbe wa Kamati Kuu ya Chadema wakiendelea na kikao hoteli ya Bahari Beach jijini Dar es Salaam cha kuwajadili Halima Mdee na wenzake 18 wanaotuhumiwa kwa usaliti wa chama kwenda kuapishwa kuwa wabunge wa viti maalum. #MwanaHALISIDigital https:View attachment 1635850View attachment 1635851View attachment 1635852View attachment 1635854
Hao wasaliti wameona aibu hawana lolote LA kujibu kunguni wale
 
Executive decision
Wawafukuze wote, ccm iwachukuwe nakuwapa uanachama.

Endapo cdm itachelewa ... itarajie maumivu makali na kitadhoofishwa sana.

Ili cdm ibakie juu na heshima, hadhi, weledi na ili iendelee kukubaliana zaidi.

Chama kiwafukuze wote na yule wa mpanda. Wasiichelewe.
yaani unaonyesha kiwango cha wivu ulionao! Wa Mpanda alifanya kampeni ya kushindwa? mara paap akashunda au? bila kupambania katiba! Haya ni maigizo tuu. Serikali na nchi wala havitasimama, waacheni hao walau tupata hadhira ya kupaza sauti !
 
Hoja ni kwamba pamoja na kuletewa Lowassa hamkuacha kusapoti Cdm,kwa hiyo hata huna sababu ya kutia mikwara ya kuacha kusapoti chadema kama hao unaoita wasaliti wakiachiwa tu.

Tuliendelea kuisupport cdm maana kosa moja haliachi mke. Na cdm uchaguzi huu hawakurudia tena kosa la kuleta wagombea wasio na ridhaa ya wanachama.
 
CDM wasipepese macho hapa, ni kuwafukuza tu hawa wahalalishaji haramu.

Ukiona nzi wa kijani wanaruka ruka Kwa furaha ujue kuna matunda yameoza au mzoga.

Ondoa mzoga mazingira yatulie watu wapate oksjeni maisha yaendelee
 
Muda mfupi kabla Kamati kuu CHADEMA kuwahoji wanachama wake walioapishwa kuwa wabunge wa viti maalum, wanachama hao wamesisitiza kutotokea mbele ya kamati kuu wakidai kupokea vitisho toka kwa viongozi na wanachama wa CHADEMA wakihofia usalama endapo watafika ofisi za chama hicho.
--
Awali Baraza la Wanawake wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (BAWACHA) leo waliandamana katika ofisi za Makao Makuu ya chama hicho zilizopo Kinondoni Dar es Salaam, kushinikiza kutowahitaji wabunge Halima Mdee, Ester Bulaya na wengine walioapishwa viti maalum.

Updates

PICHA: Wajumbe wa Kamati Kuu ya Chadema wakiendelea na kikao hoteli ya Bahari Beach jijini Dar es Salaam cha kuwajadili Halima Mdee na wenzake 18 wanaotuhumiwa kwa usaliti wa chama kwenda kuapishwa kuwa wabunge wa viti maalum. #MwanaHALISIDigital https:View attachment 1635850View attachment 1635851View attachment 1635852View attachment 1635854

Sasa si wangewasiliana na IGP Sirro ili awape ulinzi wanapokuwa wanapokuwa wanaelekea kwenye kikao kujitetea?

Kutishiwa usalama wao Hakupo Bali ni kisingizio tu...

Ukweli ni kuwa hatua yoyote itakayochukuliwa na chama chao (ambayo obviously ni kuvuliwa uanachama), dola imewahakikishia kuwa wataendelea kuwa wabunge tu...!

Andiko la Yericko Nyerere lina maana sana. CHADEMA waendelee mbele. Hakuna sababu ya kulea watovu wa nidhamu ndani ya chama wanaouza utu wao kwa fedha..

Bahati mbaya kwa dola ni kuwa, CHADEMA wakisimama kwenye msimamo wao na kua - bide ktk principles za uendeshaji wa chama, lengo la Magufuli na CCM litagonga mwamba spectacularly..

Mwafaka hapa ni kukaa mezani tu kwa ajili ya mwafaka...
 
kama kweli walicho kifanya kina Mdee na wenzake ni "usaliti" sasa tujiulize je? tunauhakika gani kwa viongozi walio baki kuwa sio wasaliti watarajiwa?! maaana hakuna aliye wahi kutarajia wala kufikiria juu ya haya yaliyo tokea,
nasisitiza mwenyekiti ajiuzulu mara moja.
 
Kama wanatishwa na wao wakimbilie wakaishi kwenye makazi ya balozi wa Ujerumani.
 
Back
Top Bottom