Halima Mdee na wenzake 18 wakata Rufaa CHADEMA

Wabunge wa viti maalumu kupitia Chadema mh Halima James Mdee na wenzake 18 wamekata rufaa kupinga kuvuliwa uanachama na kamati kuu ya chama hicho.

Source Mwananchi

My take; Hongereni kwa kuzingatia muda.

Maendeleo hayana vyama!
Mbowe kawaomba wakate rufaa ili awasamehe aendelee kupata michango.
 
Chu..!!!kwani kafulira sikuhizi unataka kusema hana cheo?..😢😲😲
 
Wanachoweza kwa sasa ni kucheza zile picha pendwa tu siasa imeshawatupa mkono

Sent from my Nokia 5.1 Plus using JamiiForums mobile app
 
Ukiona adui amebadilika ghafla kuhitaji uwe rafiki yake jitathmini
 
Njaa mbaya sana sana

Hao wameshapotea kisiasa na kujishushia heshima...
Hayo maneno yako sahau kabisa kwa mwanasiasa,nisawa na kumpigia mbuzi gitaa tu,na kumbuka tu kwamba hapa Tz hakuna mwanasiasa anayepigania maendeleo yako wote nikwaajili ya maslahi yao na familia zao
 
Yaan kwangu usaliti ni dhambi kuu kuliko zote. Ni bora uniue kabisa nisiwepo niendelee kushuhudia mambo yako. Yaan ukanisaliti nakukata maisha. Sitaki tena asilani abadani kujihusisha na wewe kinamna yoyote. Kiujumla Mdee na genge lake wameshapoteza ramani ya siasa. Hata wakasamehewa na wakabaki yaani hawana tena ule mvuto.

Kama CHADEMA watawasamehe basi wajue sisi hatuko nao tena. Naamini pia hili limeshapita. Msamaha ulipaswa kuombwa pale walipoitwa kujielezea mbele ya kamati na si kusubiri mpaka maaumuzi ndo waje omba msamaha. Sawa ni haki yao kukata rufaa lakini sioni mantiki yoyote itakayobadilika
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…