Halima Mdee na wenzake 18 wakata Rufaa CHADEMA

Halima Mdee na wenzake 18 wakata Rufaa CHADEMA

Wabunge wa viti maalumu kupitia Chadema mh Halima James Mdee na wenzake 18 wamekata rufaa kupinga kuvuliwa uanachama na kamati kuu ya chama hicho.

Source Mwananchi

My take; Hongereni kwa kuzingatia muda.

Maendeleo hayana vyama!
Mbowe kawaomba wakate rufaa ili awasamehe aendelee kupata michango.
 
Njaa mbaya sana sana

Hao wameshapotea kisiasa na kujishushia heshima

Wametanguliza maslahi ya familia na matumbo yao mbele

Hata wakiwa ccm hao ni wasaliti tu

Muangalie David Kafulila bosi wake alimwambia usigombee yeye kwa kiburi alichotoka nacho NCCR mageuzi akagombea ubunge

Covid 19 hilo ni kundi hatari ambalo watoto watakuja kufundishwa kwenye sheria kama reference ya sheria kuvunjwa za nchi
Chu..!!!kwani kafulira sikuhizi unataka kusema hana cheo?..😢😲😲
 
Hiyo rufaa wamelazimishwa na nani kuikata?

Inawezekana wanaleta maigizo, au walikuwa wanasubiri maelekezo toka kwa waliowatuma, au ni dhamira zao binafsi ndio zimewasukuma kusubiri kukata rufaa siku ya mwisho?

Kutokana na hayo maswali hapo juu nina doubt sana na dhamira yao kwenye hii issue, inawezekana walitaka kunyamaza siku ziishe bahati mbaya rumours za wanataka kwenda ACT ndio zikawasukuma kukimbilia kukata rufaa.

Hao wanawake huu mchezo wao wameshindwa kuucheza kwa kutumia akili kabisa, hilo kundi lao halina kiongozi mwenye vision.
Wanachoweza kwa sasa ni kucheza zile picha pendwa tu siasa imeshawatupa mkono

Sent from my Nokia 5.1 Plus using JamiiForums mobile app
 
Ukiona adui amebadilika ghafla kuhitaji uwe rafiki yake jitathmini
 
Njaa mbaya sana sana

Hao wameshapotea kisiasa na kujishushia heshima...
Hayo maneno yako sahau kabisa kwa mwanasiasa,nisawa na kumpigia mbuzi gitaa tu,na kumbuka tu kwamba hapa Tz hakuna mwanasiasa anayepigania maendeleo yako wote nikwaajili ya maslahi yao na familia zao
 
Yaan kwangu usaliti ni dhambi kuu kuliko zote. Ni bora uniue kabisa nisiwepo niendelee kushuhudia mambo yako. Yaan ukanisaliti nakukata maisha. Sitaki tena asilani abadani kujihusisha na wewe kinamna yoyote. Kiujumla Mdee na genge lake wameshapoteza ramani ya siasa. Hata wakasamehewa na wakabaki yaani hawana tena ule mvuto.

Kama CHADEMA watawasamehe basi wajue sisi hatuko nao tena. Naamini pia hili limeshapita. Msamaha ulipaswa kuombwa pale walipoitwa kujielezea mbele ya kamati na si kusubiri mpaka maaumuzi ndo waje omba msamaha. Sawa ni haki yao kukata rufaa lakini sioni mantiki yoyote itakayobadilika
 
Back
Top Bottom