Basi, kama ni muigizaji kiasi kile anastahili tuzo ya uigizaji.
Mtu kuigiza hadi unavunjwa viuongo kikwelikweli; sijawahi ona mwigizaji wa namna ile.
Niliposikia Mbowe akisema angependa mrithi wake awe ni kutoka BAWACHA, nilidhani alikuwa akimlenga Halima; kunbe sio? Nani basi?
Juhudi zote zile alizokuwa akizifanya hadi Bungeni, ilikuwa ni maigizo?
Lakini pia tukubali kuwapa sifa zao watu wa CCM waliofanikiwa kumrubuni. Kwanza mtu ungeanzia wapi kumsogelea Halima na kuanza kulainisha kirahisi vile? Yaani kukosa ubunge tu, tena kwa kunyang'anywa kwa nguvu, ndiyo ikawa sababu rahisi ya kumlainisha kirahisi vile Halima na akina Ester wawili?
Hawa mabinti wameingia katika historia ya usaliti, itakayowaandama maisha yao yote. Sasa wanazidi kujidhalilisha kwa haya wanayoendelea kuyafanya, huku wakiwa nje ya chama.
Matumaini ya wengi baada ya mkasa huu wa Halima na wenzake ni kwamba CHADEMA imefuzu. Imeviruka vihunzi vyote kwa ufanisi mkubwa. Chama hakijawahi kujitakasa kuliko kilivyojitakasa wakati huu. Kazi kwenu sasa kuzidi kukiimarisha chama hasa huko vijijini na mitaani.
Sasa hivi hakuna asiyejua uwepo wa CHADEMA tena ndani ya nchi hii.
Mwisho: ushauri wangu. Tazameni kwa makini sana sera zenu. Kuna baadhi ya sera hizo haziuziki kabisa kwa jamii ya waTanzania. Zitazameni kwa makini mzirekebishe panapotakiwa.