Halima Mdee na wenzako bado milango iko wazi, ‘msinyee kambi’

Halima Mdee na wenzako bado milango iko wazi, ‘msinyee kambi’

Kamati Kuu ya Chadema imewapa siku 30 Wabunge wa Viti maalumu waliovuliwa uanachama za kuomba radhi.

Huu ni muda mwafaka kwao wa kutulia na kutafakari kwa kina kilichotokea, wasiharakishe kutoa matamko, ni kipindi cha kupima faida na hasara walizopata au watakazopata kutokana na maamuzi waliyofanya, kipindi hiki wawe waangalifu zaidi.

Biashara ya siasa ni tofauti na biashara zingine, inahitaji sana trust ya watu hasa waliokuzoea, kipindi hiki wale maadui wao kisiasa waliokuwa wanaona wanafanikiwa watajitokeza na kujifanya wako karibu yao, watawakarimu kwa kila kitu, watawalipia usafiri, hoteli, watawaandalia press conference na kuelekezwa cha kuongea.

Mifano ya kujifunza ipo mingi, kwa uchache Lipumba, Mrema, Mbatia, Kabouru na Slaa, viongozi hawa baada ya kutofautiana na vyama vyao waliandaliwa press conferences na waliokuwa mahasimu wao, Lipumba hadi alipelekwa Kigali kupumzika kwa gharama zao lkn ndio ukawa mwanzo wa mwisho wao kisiasa.

Kitu cha msingi ninachotaka kuwashauri, kama bado walikuwa na mawazo ya kuendelea kuwa Chadema lkn kutokana na hili au lile wakakengeuka basi waombe radhi natumaini chama bado kinawapenda kitawasikiliza, lakini kama wameamua kuachana na Chadema bado sio mbaya lkn sio sahihi kuanza kuulaumu uongozi uliowalea, kwa sababu hata wanakokwenda kuna uongozi nao unaweza kuhisi kuna siku watauponda kama wanavyouponda uongozi wa Chadema.

Kwa sisi wazoefu wa interview ambao kazi yetu ya kila siku ni kutafuta kazi kuna swali huwa tunakutana nalo ‘kwanini uliamua kuacha kazi kwenye kampuni uliyotoka’ ukisema management ilikuwa inakunyanyasa hupati kazi.

Nawakumbusha tena msinyee kambi au msitukane mamba kabla ya kuvuka mto.

Nawatakia heri katika maisha yenu mapya ya kisiasa.
Wameshafanya maamuzi tayari halafu wewe unawashauri watafakari.Watafakari nini sasa?
 
Itakuwa walipokea hizo taarifa wakiaminishwa kuwa zina baraka ya chama chao au wametishwa, sa kitu gani kinamfanya Ndugai kwamba lazima hawa wabunge wa kuteuliwa tena wa chadema waingie Bungeni?

Hivi hana taarifa kuwa Chadema hawautambui uchaguzi walioufanya Tume ya Kileja kuwa vigezo vyake kuhisabika kama uchaguzi huru na wa haki na wa amani havikutimia? Yaani hata Magu atamshangaa huyu Ndugai.
Kwa nini wasitamke wazi wazi kuwa wametishwa au kwa nini wasingethibitisha kwanza?
 
Chadema inajikaanga na mafuta yake yenyewe.

Misimamo mikali isiyo na tija, ndiyo chanzo cha yote haya.

Hawakuwa na sababu ya kuweka misimamo mikali namna hii huku wakijua wazi kuwa haina faida yoyote.

Walisusa uchaguzi wa wenyeviti wa mitaa, Sijui hata walichotarajia. Ila maisha yanaendelea kama kawaida.

Kwa sasa chadema isitarajie kukubalika kama zamani hadi viongozi wote wajiuzulu,waje wapya na mitazamo chanya.Kwa sasa mmefeli kabisa katika sayansi ya siasa.Hamuwajui watanzania,mnawaletea masuluhisho kutoka nchi nyingine, watanzania watabaki kuwa watanzania,na hivyo suluhu zozote zilenge muktadha wa sifa na tabia za watanzania.Hivi mnavyokwenda ni sawa tu na kujikaanga na mafuta yenu wenyewe
Mkuu waache wajiteketeze wenyewe. Ikifika 2025 watapata feedback zaidi ya 2020!
 
CHADEMA bado wanawahitaji sana wabunge 19, zaidi ya hao wabunge wanavyoihitaji CHADEMA
 
Itakuwa walipokea hizo taarifa wakiaminishwa kuwa zina baraka ya chama chao au wametishwa, sa kitu gani kinamfanya Ndugai kwamba lazima hawa wabunge wa kuteuliwa tena wa chadema waingie Bungeni?

Hivi hana taarifa kuwa Chadema hawautambui uchaguzi walioufanya Tume ya Kileja kuwa vigezo vyake kuhisabika kama uchaguzi huru na wa haki na wa amani havikutimia? Yaani hata Magu atamshangaa huyu Ndugai.
Chadema ndio nani mpka atambue uchanguz ????
 
Ndio maana ya kutafakari wachuje ya kina Ndugai na chama.
Kama ni kweli viongozi wakuu wa chadema hawakuwa na taarifa za uteuzi wao, basi walishachagua tangu siku walipoamua kula kiapo
 
Wewe akili yako haina akili ,uchaguzi wa serikali za mitaa walisusia na wakashiriki uchaguzi mkuu walichokipata ni kipi? Si ni bora wangesusia kama a wali? Nani asiejua kuwa hapakuepo na uchaguzi serikali za mitaa na uchaguzi mkuu?
Kwa hiyo chadema inakurupukaaa sanaaa mkuuu
 
Siasa sio kama shule ya msingi kwamba unachapwa na kuambiwa uombe radhi. Mwanasiasa dhahifu tu ndio ataomba radhi baada ya kufukuzwa. Ukitaka uanasiasa wako ufe basi omba radhi baada ya kufukuzwa chama. Hapa pigia mstari neno KUFUKUZWA CHAMA. Ni wajinga tu wataendelea kung'ang'ania chama KILICHOWAFUKUZA, na huo utakuwa mwisho wa siasa zao ukiachia mbali huru wao na kukubalika kwao ndani ya chama walichofukuzwa.
 
Back
Top Bottom