Halima Mdee na wenzako bado milango iko wazi, ‘msinyee kambi’

Halima Mdee na wenzako bado milango iko wazi, ‘msinyee kambi’

Kamati Kuu ya Chadema imewapa siku 30 Wabunge wa Viti maalumu waliovuliwa uanachama za kuomba radhi.

Huu ni muda mwafaka kwao wa kutulia na kutafakari kwa kina kilichotokea, wasiharakishe kutoa matamko, ni kipindi cha kupima faida na hasara walizopata au watakazopata kutokana na maamuzi waliyofanya, kipindi hiki wawe waangalifu zaidi.

Biashara ya siasa ni tofauti na biashara zingine, inahitaji sana trust ya watu hasa waliokuzoea, kipindi hiki wale maadui wao kisiasa waliokuwa wanaona wanafanikiwa watajitokeza na kujifanya wako karibu yao, watawakarimu kwa kila kitu, watawalipia usafiri, hoteli, watawaandalia press conference na kuelekezwa cha kuongea.

Mifano ya kujifunza ipo mingi, kwa uchache Lipumba, Mrema, Mbatia, Kabouru na Slaa, viongozi hawa baada ya kutofautiana na vyama vyao waliandaliwa press conferences na waliokuwa mahasimu wao, Lipumba hadi alipelekwa Kigali kupumzika kwa gharama zao lkn ndio ukawa mwanzo wa mwisho wao kisiasa.

Kitu cha msingi ninachotaka kuwashauri, kama bado walikuwa na mawazo ya kuendelea kuwa Chadema lkn kutokana na hili au lile wakakengeuka basi waombe radhi natumaini chama bado kinawapenda kitawasikiliza, lakini kama wameamua kuachana na Chadema bado sio mbaya lkn sio sahihi kuanza kuulaumu uongozi uliowalea, kwa sababu hata wanakokwenda kuna uongozi nao unaweza kuhisi kuna siku watauponda kama wanavyouponda uongozi wa Chadema.

Kwa sisi wazoefu wa interview ambao kazi yetu ya kila siku ni kutafuta kazi kuna swali huwa tunakutana nalo ‘kwanini uliamua kuacha kazi kwenye kampuni uliyotoka’ ukisema management ilikuwa inakunyanyasa hupati kazi.

Nawakumbusha tena msinyee kambi au msitukane mamba kabla ya kuvuka mto.

Nawatakia kila la heri katika maisha yenu mapya ya kisiasa.
Bado ni wàbunge na hawataomba radhi
 
Ebu nikumbushe bado Kafulila yupo NCCR, nini kilimuondoa baada ya radhi yake?
Mkuu kuomba radhi hakuna uhusiano wowote na makosa yake ya baadae. Hatupo perfect lakini kuomba radhi ni ukomavu whether una kosa au lah
 
Mkuu kuomba radhi hakuna uhusiano wowote na makosa yake ya baadae. Hatupo perfect lakini kuomba radhi ni ukomavu whether una kosa au lah

Kuomba radhi wakati haujafanya kosa ni utumwa na ndio kinachoitesa nchi yetu tangu awamu ya tano ianze. Kila anayeupinga utawala anatakiwa awe apologetic na approve inferior kwa mtawala. Ukomavu ni kusimamia kile unachokiamini hata kama dunia mzima itakupigia kelele ukibadirishe, ukomavu ni kutokubali uonevu na kunyanyaswa ili kumlidhisha anayekuonea au anayekunyanyasa. If you don't stand for what you believe you definitely stand to lose yourself. Dangerous for yourself and others.
 
Kamati kuu iliwapa nafasi ya kuomba radhi
 
Back
Top Bottom