Halima Mdee na wenzako bado milango iko wazi, ‘msinyee kambi’

Wameshafanya maamuzi tayari halafu wewe unawashauri watafakari.Watafakari nini sasa?
 
Kwa nini wasitamke wazi wazi kuwa wametishwa au kwa nini wasingethibitisha kwanza?
 
Mkuu waache wajiteketeze wenyewe. Ikifika 2025 watapata feedback zaidi ya 2020!
 
CHADEMA bado wanawahitaji sana wabunge 19, zaidi ya hao wabunge wanavyoihitaji CHADEMA
 
Chadema ndio nani mpka atambue uchanguz ????
 
Ndio maana ya kutafakari wachuje ya kina Ndugai na chama.
Kama ni kweli viongozi wakuu wa chadema hawakuwa na taarifa za uteuzi wao, basi walishachagua tangu siku walipoamua kula kiapo
 
Wewe akili yako haina akili ,uchaguzi wa serikali za mitaa walisusia na wakashiriki uchaguzi mkuu walichokipata ni kipi? Si ni bora wangesusia kama a wali? Nani asiejua kuwa hapakuepo na uchaguzi serikali za mitaa na uchaguzi mkuu?
Kwa hiyo chadema inakurupukaaa sanaaa mkuuu
 
Siasa sio kama shule ya msingi kwamba unachapwa na kuambiwa uombe radhi. Mwanasiasa dhahifu tu ndio ataomba radhi baada ya kufukuzwa. Ukitaka uanasiasa wako ufe basi omba radhi baada ya kufukuzwa chama. Hapa pigia mstari neno KUFUKUZWA CHAMA. Ni wajinga tu wataendelea kung'ang'ania chama KILICHOWAFUKUZA, na huo utakuwa mwisho wa siasa zao ukiachia mbali huru wao na kukubalika kwao ndani ya chama walichofukuzwa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…