Kwa mujini Wa katiba ya chadema ukienda mahakamani kukishitaki chama kwa maamuzi kiliyofanya unapoteza wanachama wako directly. Zito alipoteza wanachama directly
Wakubali tu kuwa ukweli siku zote uta prevail tu hata ukifunikwa vipi.
Sheria ndio huamua haki na huhifadhi haki ni kwamba walichelewesha tu maamuzi ila kimsingi regardless Mbowe aliamua kuwakomoa but ndo katiba inavyotaka kuwa wasiendelee kuwa wabunge as long as sio wanachama. Huu ukweli its time waukubali.
Alitaka kuwakomoa vipi? Wameachiwa mwaka mzima wa kuwa wabunge au kusahihisha makosa yao. Wao hawakutaka kuachia ubunge. Mbowe kawakomoa kivipi? Unadhani wanachama wangelielewa Baraza lao kama lingeamua kuwasamehe na kuwaacha waendelee na ubunge wao? Kupanga ni kuchagua na wamevuna walichopanda.
Sasa wako huru kwenda Mahakamani, kujiunga na chama kingine, kustaafu au kujirekebisha. Wakiweka kiburi pembeni wanaweza kuomba msamaha na kuomba uanachama upya.
Ila kwa vile Tulia hawapendi basi nafasi zao zitatangazwa kuwa wazi fasta.
Huu uamuzi kama ukifanyika ndio unaenda kuwa mwanzo wa tatizo jingine, hapa zitakuja assumptions za kila aina toka kwa maadui wa Chadema.
Hapa utatumika ukanda, ukabila, mahusiank, dini, na sababu nyingine zote ili kuhalalisha kina Mdee wameonewa ili wawekwe watu wao.
Nawashauri Chadema wabaki na msimamo wao wa mwanzo, kutoyatambua matokeo ya ubunge na Urais wa 2020 na kutopeleka wabunge bungeni, kama shida ni ruzuku, waendelee kuokoteza mitaani kama wanavyofanya.
Kwangu ni bora kupitia machungu ili kulinda heshima, kuliko kubadili msimamo wako na kupata kingi huku ukijipotezea heshima, hapa wasiyumbe kimsimamo.
Hakuna namna wanaweza "substitute" maamuzi yao ya mwanzo kwa kupeleka majina mengine bungeni ikiwa athari za uchaguzi ule bado zipo mpaka leo, hata kama serikali imebadilika.
Dar es Salaam. Aliyekuwa mwanachama wa CHADEMA, Halima Mdee amesema hakukuwa na uhuru kwa wajumbe wa Baraza Kuu la chama hicho katika upigaji wa kura na kwamba, kilichofanyika ndani ya Baraza hilo ni uhuni. Na Mbowe anajua ni Uhuni. Nitaongea siku nyingine kwa Urefu leo sio siku mwafaka. Mimi Halima Mdee ni CHADEMA na nitaendelea kuwa chadema
HALIMA MDEE NA WENZAKE 18 WAFUKUZWA RASMI CHADEMA Baraza Kuu la #CHADEMA limezitupilia mbali Rufaa za Halima Mdee na wenzake 18 wakipinga kufukuzwa uanachama na Kamati Kuu ya chama hicho kwa kukubali kwenda kuapishwa na kuwa wabunge wa Viti Maalumu bila baraka za chama ====== UPDATE: Halima...
Dar es Salaam. Aliyekuwa mwanachama wa Chadema, Halima Mdee amesema hakukuwa na uhuru kwa wajumbe wa Baraza Kuu la chama hicho katika upigaji wa kura na kwamba, kilichofanyika ni uhuni.
Mdee ambaye amepata kuwa mbunge wa Jimbo la Kawe na Katibu wa Baraza la Wanawake wa Chadema, Bawacha, ni miongoni mwa makada walifukuzwa baada ya Bazara Kuu kubariki uamuzi wa Kamati Kuu ya Chadema kuwafukuza ndani ya chama kwa kukubali kwenda kuapishwa na kuwa wabunge kinyume cha matakwa ya chama hicho.
Matokeo ya jumla
Idadi ya wajumbe 423
Waliokubalina na maamuzi ya Kamati ya kuwafukuza Uanachama ni 413 sawa 97.6%
Wasiokubaliana na uamuzi wa Kamati kuu ni 5 sawa na 1.2%
Hata ongea yake tu imekaa kihuni. Aliyemharibu Mdee ni huyo Bulaya.
Ninachowasharuri wakubaliane na kufukuzwa kwao, watoke bungeni then warudi kuomba msamaha wakiwa hawana nafasi yoyote.
Halima atafute chama kingine, mahakamani atapoteza vingi, kwa Sasa sio mwanachama ataenda kupambana Kama raia wa kawaida kwa ajili gani?. Akubali ameshindwa na Hana influence Tena CHADEMA. Atafute platform nyingine. Kuendeleza mapambano ambayo huyawezi ni kupoteza muda.
Kwanza walishaga toa msimamo kwamba hawapeleki wabunge wa viti maalum kwa kuwa uchaguzi ulikuwa batili Sasa swala la kusema wataselect new mps hilo ni ngonjera tu
Hata ongea yake tu imekaa kihuni. Aliyemharibu Mdee ni huyo Bulaya.
Ninachowasharuri wakubaliane na kufukuzwa kwao, watoke bungeni then warudi kuomba msamaha wakiwa hawana nafasi yoyote.
Mnamuonea Bulaya. Halima aliamini yeye ni zaidi ya chama chake. Aliamini Bawacha itakuwa upande wake akatingisha kiberiti. Matokeo ndio haya. Bulaya hana makosa.
Wanaweza kwenda Mahakamani wakaomba order ya status quo pending main case kama watakuwa wamefile na wamebaini katiba ya CDM haikufuatwa kisawasawa wakati wanatimiliwa
Wakienda mahakamani hawatalipwa tena na bunge, mpaka labda washinde kesi ndio watalipwa malimbikizo yao ya mishahara! ni sawa na kufukuzwa kazi, ukipinga mahakamani hulipwi mshahara mpaka ushinde kesi....
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.