the truecaller
JF-Expert Member
- May 8, 2019
- 809
- 940
Hao wote na hivyo vyeo vyao wakiwa nje ya CCM hawana tofauti na Mmachinga tu na wala hawana uwezo wa kufanya lolote lile.
Ila wakiwa ndani ya CCM vyeo vyao ndio vinaweza kuwasaidia kujimwambafai.
Tujiulize hawa wazee wastaafu nje ya CCM kwanini pamoja na vitisho vya awamu ya 5 hawakujitokeza kuomba 'msamaha' ni nini kinawafanya kujiamini hivi wakati wastaafu kama Edward Lowassa, Fredrick Sumaye n.k wameamua kurudi 'nyumbani'.
Je kuna CCM "mtandao' iliyo nje ya hii ya awamu ya 5 na inataka pia ipo tayari kwa mapambano na hawa CCM 'wakuja'.
Hapo hamna hata kujiuliza mkuu,hao wote ni bure nje ya CCM.
Yaani hao wote uliowataja ukiwajumlisha kwa pamoja hawafikii nguvu za Lowassa enzi zake akiwa anatisha lkn ametulizwa tuli na kuunga mkono juhudi sembuse hao.
Hebu mkuu niambie Kinana,Makamba,Membe wana influence gani hata kwa wananchi wa kawaida?
Tena atayamaliza ceremonoslyMzee makamba atayamaliza tu
Mwakani atakuwepo jukwaani anapigia kampeni Ccm
Alidai JAKAYA alikuwa anawabatiza WAPINZANI KWA MAJI. Ila JPM atawabatiza kwa MOTO. Alishangiliwa sana siku ile. Alikuwa hajui kama JPM ni kama MTEGO WA PANYA. Badala ya kusaidia KUUTEGUA, akawa anajiona YEYE HAUMUHUSU. Leo hii, kanaswa mwenyewe!Unabii Wake Umetumia Vyema Kabisa.
Kwasasa Makamba Ni Nabii Kamili.
Ila sikumbuki Kama alisema,
JPM atawabatiza kwa Moto au
JPM atatubatiza kwa Moto.
Sent using Jamii Forums mobile app
Mshindi shindano la mswahili ajalipwa,halafu wanataka kuanzisha lingine.Tuendelee kulima bamia Mbutu huku tukisuburi urithi wa ardhi.Mzee wetu Yusuph Makamba,almaarufu nabii wa ubatizo wa moto,amenasa kwenye tanuru la unabii wake.
Hana namna ya kujinasua,bali anatakiwa kuonja kikombe hicho ambacho kwa hakika kiko mbele yake.
Je akitoka kunywa kikombe cha moto atakuwa kabadilika?
Amesema hoja hujibiwa kwa hojaAnaetafutiwa tyming ni mmoja tu hao wengine ni wasindikizaji. Hapo si mwingine bali "Niguse Ninuke" Makamba ni Mzee wa Kiswahili huyo anataka kumuuza/kuwauza mwenzie/wenzie.
Sent using Jamii Forums mobile app