Halmashauri kuu ya Taifa ya CCM yawaita ili kuwahoji Kinana, Makamba na Membe

Halmashauri kuu ya Taifa ya CCM yawaita ili kuwahoji Kinana, Makamba na Membe

Inamaana hao wahusika watatu hawakuhudhuria kikao cha halmashauri hiyo jana?.au sio wajumbe
 
Kuna watu wana roho ngumu aisee! Hivi Makamba Jr unafurahiaje wewe kusamehewa wakati baba yako anaenda kubatizwa?
 
vposterior,
Sasa na wewe unajiita Great Thinker au unaendeleza majungu tu bila ushahidi. Unaonyesha nia ya kugombea CCM sasa inawahusu nini Watanzania. Sisi ambao hatuna vyama haituhusu, wale wanaopigiwa kura wapo kwenye ballot paper kama humo haituhusu. Ungetueleza maswala ya mgombea huru ningekuelewa kidogo. FYI democrasia iliyopo Tanzania ni kubwa sana ndio sababu upo hapa unabwata. Huo wendawazimu wako kaa nao huko kwenu kwanza hata hufahami jinsi TISS, Jeshi, mahakama au Bunge linavyofanya kazi utaweza kweli kujadili vitu complicated? BTW prove kwamba wapiga kura wanawekewa mtutu wa bunduki? Then mambo ya CCM kudukuana hayatuhusu.
 
Mojawapo ya vitu ambavyo Magufuli anavilazimisha kufanyika sasa hivi ni kuwa asiwepo mtu ambaye "hagusiki" ama iwe kwa sababu ya cheo chake, hadhi yake au historia yake. Ila ukishatengeneza mazingira ya namna hii hata huko mbeleni watu wengine nao watakuja kuitwa vile vile bila kujali hadhi, cheo au historia waliyowahi kuwa nayo.

Anyone mwenye cheo cha urais akiamua kuwa bully anaweza kuwa bully, Magufuli is a bully. It is not about ujasiri, rather kwake ni egoism!. Kwamba nina nyundo kubwa ninaweza kumpobda nalo yeyote. Waliomtangulia walikuwa wakifanya lakini kwa staha!.

Magufuli angekuwa haangalii mtu usoni leo hii Makonda angekuwa jela!

Kwa hiyo mzee mwanakijiji mfano wako ni mfu!
 
Wazee waliompeleka Magufuli Ikulu?

Magufuli kawakosea heshima wazee.
Kila siku huwa nasema. Hakuna watu wabovu kutawala nchi yetu kama hawa Chadema na wapiga debe wake. Wewe unataka kutuambia kuwa mwanznchi anayesaidia kiongozi kupata nafasi basi hata kama akikosea basi ''asikikosewe heshima'' kwa kuulizwa. Unadhani kuwa kumsaidia kiongozi wakati wa kampeni basi ni tiketi ya kutoguswa kwa chochote utakachofanya. Upinzani Tanzania ni wabovu mara kumi kuliuko CCM. Ndiyo maana yale yale wanayopigia kelele huwa wanayafanya tena kuliko hata CCM. Uenyekiti wa vyama hawataki kuachia fedha wanatumia hovyo kwa kukodi ndege!
 
Hawana la kuwafanya wale wazee mbali na kuwasamehe bila masharti yoyote.
 
Nyie makanali wa Jeshi na watumishi wa CCM, hamuwezi kudhalilishwa namna hii na nyie mkaenda kupiga magoti.
Tena ni wajeda walio kamilika, wasiyumbishwe na raia hao wa CCM, mmefanya mengi kupigania nchi hii mpaka tukawa hapa tulipo wapotezeeni.

Muhojiwe kwani nyinyi ni majambazi? Yaani wanafuata shinikizo kutoka kwa Musiba? yeye Musiba nani alimtuma? watu wanaweza kuigiza sauti zetu wasanii ni wengi! hata km mlisema hayo hamkuwa na nia mbaya mbona Mungu wanamsema!

Kwa umri wenu hakuna cha kupoteza hata mkifukuzwa uanachama, wao ndo waombe msamaha!
 
Watafuatia January, Nape na Ngereja!

Ohh.....sorry kumbe wamesamehewa.........CCM ni chama kikubwa sana!

Maafande wastaafu wanaipenda sana CCM nakumbuka Kamishna mkuu mstaafu wa Magereza awamu ya mzee Mwinyi ndugu yetu Jumanne Mangala alikuwa Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Pwani!
january, ngeleja na nape wamefanya kosa moja na wazee. wao wamefutiwa wenzao wameitwa kwenye kikao. akili za mwenyekiti wa CCM zinashida mahali fulani, dishi limecheza kidogo. nawaza tu
 
january, ngeleja na nape wamefanya kosa moja na wazee. wao wamefutiwa wenzao wameitwa kwenye kikao. akili za mwenyekiti wa CCM zinashida mahali fulani, dishi limecheza kidogo. nawaza tu
Inawezekana wewe dish ndio limecheza, umeshaambiwa maamuzi ya kikao cha halmashauri kuu ya chama, sasa mwenyekiti unamuongelea vibaya as if alijifungia pekee yake na akatoa maamuzi
 
Huwezi kuweka kesi ambayo ushahidi wako ni kerekodi lakini mrekodi mwenyewe ni wa siri na hataki kujulikana.

Sasa je tuna ushahidi gani kwamba rekodi hizo kuna maneno ambayo yamefutwa makusudi, je tunajuaje kama warekodi walikuwa hawana nia zao binafsi.

Kama una mrekodi mtu masaa 24 kila siku huwezi kukosa maneno ya kuunganisha au kuchagua sentensi fulani tu kupendezesha story yako.

Hivyo kwa washitaki wa Kinana, Makamba, na Membe wajiandae kueleza nani amerekodi simu zao na watoe ushahidi kwamba hakuna maneno yamefutwa.

Bila hivyo mtu yeyote anaweza kubambikizwa kesi.
 
Hiwezi kuweka keshi ambayo ushahidi wako ni kerekodi lakini mrekodi mwenyewe ni wa siri na hataki kujulikana!. Sasa je tuna ushahidi gani kwamba rekodi hizo kuna maneno ambayo yamefutwa makusudi, je tunajuaje kama warekodi walikuwa hawana nia zao binafsi. Kama una mrekodi mtu masaa 24 kila siku huwezi kukosa maneno ya kuunganisha au kuchagua sentensi fulani tu kupendezesha story yako. Hivyo kwa washitaki wa kinana, Makamba, na Membe wajiandae kueleza nani amerekodi simu
zao na watoe ushahidi kwamba hakuna maneno yamefutwa. Bila hivyo mtu yeyote anaweza kubambikizwa kesi.

Ushahidi unaopatikana kwa kuvunja sheria, siyo ushahidi halali.

Ukija kwangu ukafunga vinasa sauti kwa siri halafu ukanisikia namteta Magufuli huku nikiwa na mke wangu huwezi kunipeleka kikao cha maadili cha chama kwa ushahidi huo
 
Back
Top Bottom