Halmashauri kuu ya Taifa ya CCM yawaita ili kuwahoji Kinana, Makamba na Membe

Bhisumbinyama,
Mkuu nawe ni mmbeya! Kila wakati unaulizia lini nampiga mke wangu! Yanakuhusu nini?
Waache CCM wanajua ya kwao, hangaika na ya kwako!
 
Hawa lazima tuwafuatilie hatua kwa hatua kwa kuwa kwa sasa chama chao ndo kina ridhaa ya kutawala hivyo wakifanya ujinga unatuhusu na wakifanya mazuri tunanufaika. Ndo kwa sasa wanakusanya kodi zetu hao.
 
Kuna ndani ya CCM kunahitaji uvumilivu wa hali ya juu sana, nani aliota Kinana na Bashte kufanya kazi pamoja leo
 
Hapo zamani🤣
Siyo zaman, ni majuzi tu hawa walikuwa na Mgogoro na JPM. Mama aliamua kuishi na wanafiki.

JPM alisingiziwa meng sana na wanafiki hawa. Nchimbi mda wowote atatolewa na Polepole kupewa CHAMA. Pinda Makamu Mwenyekiti. 2025 Mama anapumzika Hussein Mwinyi anachukua hatamu mpaka 2035. JPM OYEYEEEEE!
 
Chama cha Mapindizi CCM kimeridhia kwa kauli moja kuwasamehe Nape, January Makamba na Ngeleje hata hivyo wamepewa onyo kali wasirudie tena kosa hilo.

Hata hivyo kimeagiza kwa kauli moja kuhojiwa kwa Makatibu wakuu wastaafu Kinana na Makamba pamoja na Waziri wa Zamani Ndugu Bernard Membe.

Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM imeagiza makatibu wakuu wastaafu wa chama hicho, Abdulrahman Kinana, Yusuf Makamba na waziri wa zamani wa Mambo ya Nje, Bernard Membe kuhojiwa na kamati ya usalama na maadili ya Taifa ya chama hicho kujibu tuhuma za kimaadili zinazowakabili.

Zaidi, soma:

FB_IMG_1576245504069.jpeg

Aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Nje, Bernad Membe
FB_IMG_1576245500230.jpeg

Yusufu Makamba Katibu mkuu wa zamani wa CCM
FB_IMG_1576245492207.jpeg

Abdulrahman Kinana Katibu mkuu wa zamani wa CCM

Sent using Jamii Forums mobile app
Mwanza. Chama Cha Mapinduzi (CCM) nchini Tanzania kinapenda kuujulisha umma wa wana CCM na Watanzania kwamba Halmashauri Kuu ya Taifa (HKT) imeketi leo Ijumaa Desemba 13, 2019 jijini Mwanza chini ya Rais John Magufuli.

Mkutano huo wa Halmashauri Kuu ya Taifa (HKT) ni wa kawaida kwa mujibu wa Katiba ya CCM. Katika mkutano huo, imewasamehe wanachama wake watatu huku wengine wakitwa kuhojiwa.

Walioitwa kuhojiwa ni makatibu wakuu wawili wa zamani wa chama hicho, Abdulrahman Kinana na Yusuf Makamba pamoja na Benard Membe.

Kabla ya Kikao cha Halmashauri Kuu ya Taifa wajumbe walifanya ziara ya kukagua miradi mikubwa ya kimkakati inayotekelezwa katika Mkoa wa Mwanza.

Wajumbe pia walipata muda wa kujadili Taarifa ya Utekelezaji wa Ilani ya CCM kwa kipindi cha Miaka Minne ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Maandalizi na maudhui ya Mwelekeo wa Sera za CCM kwa Mwaka 2020 – 2030 sambamba na Ilani ya Uchaguzi ya CCM katika Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2020.

Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa (HKT) wameazimia kwa kauli moja kupongeza Serikali ya Tanzania inayo ongozwa na Rais Magufuli na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ) inayo ongozwa na Rais Ali Mohamed Shein kwa utekelezaji mzuri wa Ilani ya uchaguzi ya CCM ambapo mafanikio makubwa ya kimaendeleo yamepatikana.

Halmashauri Kuu ya Taifa (HKT) imepokea, kujadili na kuridhia kwa kauli moja Taarifa ya Kamati ya Usalama na Maadili juu ya uamuzi wa Mwenyekiti wa CCM wa kuwasamehe wanachama walioomba radhi kwake baada ya kukiri mbele yake kufanya makosa ya kimaadili yaliyokidhalilisha chama na viongozi wake mbele ya umma.

Wanachama hao ni;-

1. Ndg. Januari Makamba (Mb)

2. Ndg. Nape Nnauye (Mb) na,

3. Ndg. William Ngeleja (Mb)

Kikao cha HKT kimewataka wanachama hao kujirekebisha na kutorudia makosa yao ama sivyo hatua kali zitachukuliwa dhidi yao kwa mujibu wa katiba, Kanuni na taratibu za Chama ikiwamo kufukuzwa uanachama.

Wakati huo huo, Halmashauri Kuu ya Taifa (HKT) imeazimia kwa kauli moja na kuelekeza kwamba wanachama wafuatao;-

1. Abdulrahman Kinana

2. Mzee Yusuf Makamba na,

3. Benard Membe

Waitwe na Kamati ya Usalama na Maadili ya Taifa ili wajibu tuhuma za kimaadili zinazowakabili kwa mujibu wa Katiba ya Chama na Kanuni ya Maadili na Uongozi.

Awali Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM (HKT) imefanya uteuzi wa majina ya Wagombea wa nafasi za Uongozi katika Chama na Jumuia kama ifuatavyo;-

1. Wagombea wa nafasi ya Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Arusha

a. Ndg. Batilda Salha Buriani

b. Ndg. Zelothe Stephen Zelothe

c. Ndg. Bakari Rahibu Msangi

2. Wagombea wa nafasi ya Katibu wa Siasa na Uenezi Mkoa wa Iringa

a. Mafanikio Paulo Kinemelo

b. Hilary Adelitius Kipingi

c. Lucas Felix Lwimbo

3. Wagombea wa nafasi ya Katibu wa Siasa na Uenezi Mkoa wa Mtwara

a. Petro Mwendo Mwendo

b. Mustafa Nguyahamba Mohamed

c. Selemani Manufred Sankwa

4. Wagombea wa nafasi ya Mwenyekiti wa Wazazi Mkoa wa Dodoma

a. Ndg. Damas Mukassa Kasheegu

b. Baraka Andrea Mkunda

c. Christopher Thomas Mullemwah

5. Wagombea wa nafasi ya Mwenyekiti wa UVCCM Mkoa wa Pwani

a. Mary Daniel Joseph

b. Fredrick Gasper Makachila

c. Samaha Seif Said

Licha ya hamasa kubwa waliyokuwa nayo wajumbe wa HKT kutokana na kazi nzuri ya Serikali ya CCM, Ndg. Magufuli amesisitiza kazi ya Urais ni ngumu sana na yeye ataheshimu utamaduni na desturi za CCM, Kanuni, Katiba ya CCM na Katiba ya Nchi na kwamba CCM ni kiwanda cha kuzalisha viongozi na kwa utaratibu ambao chama kimejiwekea kitampata mtu bora zaidi atakayepokea uongozi baada yake.

Nawashukuru sana viongozi wa Halmashauri Kuu ya Taifa (HKT) ya Chama chetu kwa kuzisimamia vizuri Serikali zetu mbili na hivyo kuwezesha kupatikana mafanikio makubwa katika Utekelezaji wa Ilani ya CCM.

Tukaendelee kujenga umoja, kuimarisha ujenzi wa Chama chetu na tunapoelekea katika chaguzi zinazokuja tukaepuke makundi, na tuendelee kuisimamia Serikali ikiwamo kukagua miradi ya kimaendeleo katika maeneo yetu, amesema Ndg. Magufuli Mwenyekiti wa CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Credit Mwananchi
View attachment 1291275View attachment 1291276

Sent using Jamii Forums mobile app
Kumbe Hawa watu kuyumbisha Viongyna usaliti ni kawaida Yao,Kwa nini isiwe nitolee Jumla?
 
Nikajua ni habari mpya
 
Back
Top Bottom