Mwanongwa
JF-Expert Member
- Feb 15, 2023
- 611
- 567
Mimi kama mkazi wa Jiji la Mbeya kuna kitu sikielewi kutoka kwa Viongozi wa Jiji hasa Idara ya Ardhi na Watu wa Mazingira wa NEMC.
Huku Mbeya katika Kata ya Nsalaga, Bonde la Uyole, Uongozi wa Halmashauri ulianzisha mradi wa viwanja vipya na kuhamasisha sana Wananchi wajitokeze kununua viwanja hivyo, kweli tulijitokeza na kununua.
Lakini kinachoendelea hivi sasa katika eneo hilo la mradi huo wa viwanja ni balaa tupu na hatari kwetu Wananchi wa maeneo hayo.
Kuna raia mmoja mwenye asili ya Uarabuni anayemiliki kampuni ya ukandarasi, naye amepewa kibali cha kuchimba mawe katika maeneo hayo, amefunga na mitambo yake ya kusaga mawe.
Kibaya zaidi siyo kuchimba tu bali anapiga baruti kwaajili ya kuvunja miamba hiyo ya mawe maana mawe ya juu tayari amekwisha yamaliza na sasa ni mwendo wa baruti tu.
Sisi tulionunua viwanja kwaajili ya kujenga tutawezaje kujenga eneo hilo wakati kuna shughuli za uchimbaji zinaendelea karibu na maeneo yetu, pia baruti ni hatari sana sababu zinarusha mawe, hivyo zinahatarisha maisha ya Watu na viumbe wengine.
Mitambo yake ya kusaga mawe inachafua hali ya hewa kila siku sababu vumbi muda wote zinatapakaa kwenye makazi ya watu na kusababisha magongwa mbalimbali kikiwemo kikohozi pamoja na mafua yasiyoisha.
Najiuliza hapa hivi wakati mamlaka zinampatia kibali huyo mwekezaji mwenye kampuni hiyo inayoitwa Narmo, ilitegemea sisi tunajengaje sasa maeneo hayo?
Upande wa pili ninyi NEMC inamaana hamuoni kama jamaa anaharibu mazingira kwa kuchimba mawe tena kwa kupiga baruti muda wote wa shughuli.
Baruti hizo zimesababisha nyufa kwenye nyumba nyingi tu za Wananchi waishio karibu na maeneo hayo ya mradi huo wa mgodi wa mawe kama wanavyouita.
Kulikuwa na ulazima gani wa kutoa kibali kuendesha shughuli hiyo ya uchimbaji wakati mnajua fika kuwa italeta shida kwa sisi Wananchi ambao tumenunua viwanja maeneo hayo.
Siyo siri Viongozi wa Halmashauri hasa Idara ya Ardhi mmetukosea sana Wananchi, pesa zetu mmechukua na mmetuletea majanga maana hatuwezi kabisa kujenga kutokana na baruti zinazopigwa, moja zinaweza kuangusha nyumba na pia tutakuwa tunalazimika kutoka kwa muda katika nyumba zetu ili kupisha baruti kupigwa.
Watu wa Reli wakague reli yao
Ndugu zangu wa mamlaka ya reli nawakumbusha kupita kukagua njia yenu ya treni sababu imepita maeneo hayo ambayo zoezi la uchimbaji wa mawe kwa njia ya kupiga baruti linaendelea, hivyo ni vyema kupita na kuikagua njia hiyo mara kwa mara ili mbeleni yasije yakatokea majanga.
Mtafutieni huyo mwekezaji eneo lingine nje ya mji ndiyo akachimbe hayo mawe na siyo hapa katika eneo ambalo mmetuuzia viwanja.