KERO Halmashauri ya Bariadi yaanzisha Dampo la Kidinda katikati ya makazi ya Wananchi

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Joined
Feb 7, 2022
Posts
2,780
Reaction score
6,607

Wananchi wa Mtaa wa Majengo, Kata ya Bariadi, Halmashauri ya Mji wa Bariadi Mkoani Simiyu wako katika wakati mgumu kutokana na harufu kali na chafu inayotoka kwenye Dampo la takataka ambalo Halmashauri imelianzisha katikati ya makazi yao.

Mbali na harufu kali, Wananchi hao wanalalamikia kitendo cha kila siku cha uchomwaji moto wa takataka zikiwemo chupa za plastiki kwenye dampo hilo na kusababisha moshi wenye harufu kali kusambaa kwenye makazi yao.

“Huu moshi unaochomwa hapa ni hatari sana, unatusumbua vibaya kila siku, moshi ni mkali, una harufu kali, kila wakati ni vikohozi, tatizo jinginge kubwa ni harufu mbaya, uchafu wote wa mji wa Bariadi unaletwa hapa, wakati wanajua hapa ni makazi ya watu,” anasema Madeleke Maduhu.


“Ikifika jioni unatamani uondoke kwenye huu mtaa, harufu ni kali, hawa watu hawana huruma hata kidogo, tunatamani Mkurugenzi aje aishi kwenye huu mtaa, aone namna wananchi tunavyoteseka na Moshi na harufu ya Dampo hili,” amesema Zacharia Limbu.

Jananja Buluba anasema kuwa katika mtaa huo, wananchi wengi hawawezi kupika Samaki, kwani inzi wanaotoka kwenye Dampo hilo wakisikia harufu ya samaki watajaa kwenye nyumba nje na ndani.

Mwenyekiti wa Mtaa huo Maduhu Nyanda anakiri uwepo wa kero hiyo, ambapo ameeleza kuwa kupitia vikao vya kamati ya maendeleo kata (WODS) wamekuwa wakipeleka malalamiko Ofisi ya Mkurugenzi na kutaka Dampo hilo kuondolewa kwenye mtaa wao lakini hawasikilizwi.

Diwani wa kata hiyo Kija Bulenya amekiri kupata malalamiko ya wananchi hao huku na kusema kuwa ni kweli dampo hilo limekuwa kero kwa wananchi wake, licha ya kuwataka wahusika waliondoe lakini bado hawajatekeleza.

Mkuu wa Kitengo cha Usafi na Udhibiti Taka Halmashauri ya Mji, Peter Subadi anasema kuwa changamoto hiyo wameiona na kama Mamlaka wameamua ndani ya wiki hii dampo hilo litafungwa rasmi.

“Lile lilikuwa dampo dogo sasa kutokana na ongezeko la watu, uchafu umekuwa mwingi, Wiki hii tunalifunga na tutaweka ulinzi hakuna mtu yeyote kumwaga uchafu eneo hilo, na tutakuja na utaratibu mwingine,” amesema Subadi.


Pia Soma:
~
Simiyu: Baada ya kulalamika Dampo kwenye makazi ya watu, viongozi watoa tangazo la kuzuia Dampo lakini waweka kifaa cha kuhifadhi taka
~ Dampo la Kidinda Bariadi linaanza kurudi, baadhi ya watu wanatupa taka usiku. Hatua zichukuliwe haraka
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…