A
Anonymous
Guest
Halmashauri ya Wilaya ya Hanang’ haijalipa fedha za stahiki kwa wakulima na wafugaji walioshiriki katika Maonesho ya Nane Nane yaliyofanyika katika Viwanja vya Themi-Njiro, Arusha, kuanzia tarehe 28 Julai hadi 9 Agosti.
Tunapowasiliana na Afisa Kilimo wa Wilaya kuhusu malipo hayo, majibu tunayopata hayaridhishi, akisema hana fedha. Pia, tunapowauliza watumishi tuliokuwa nao kwenye maonesho hayo, hatupati majibu yanayoeleweka kuhusu hatma ya malipo yetu.
Kinachotia wasiwasi zaidi ni kwamba Afisa Kilimo huyo kwa sasa anakaimu nafasi ya Mkurugenzi wa Halmashauri, hivyo tunatarajia kuwa na uwezo wa kufuatilia na kutoa ufafanuzi kuhusu fedha na stahiki zetu.
Tunaomba mamlaka husika ichunguze suala hili na kuhakikisha tunalipwa stahiki zetu kwa wakati. Tulitumia fedha zetu za mfukoni kugharamia mahitaji mbalimbali wakati wa ushiriki wetu jijini Arusha, hivyo kucheleweshwa kwa malipo hayo kunatuweka katika hali ngumu.
Tunaomba haki yetu ilindwe na mamlaka husika itoe ufafanuzi kuhusu fedha hizo pamoja na lini tutalipwa.