Halmashauri ya Kibaha Mji: Hatuhusiki mgogoro wa eneo la Matuga, Maafisa wetu walioenda huko walikuwa na mambo yao binafsi

Halmashauri ya Kibaha Mji: Hatuhusiki mgogoro wa eneo la Matuga, Maafisa wetu walioenda huko walikuwa na mambo yao binafsi

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
3,984
Reaction score
13,760
Baada ya Mdau wa JamiiForums.com kudai kuna kuna baadhi ya Mafisa wa Halmashauri ya Kibaha Mji wamekuwa wakiwasumbua Wananchi wa Matuga, Kibaha Vijijini kwa kuwatishia ili kuwaondoa kwenye makazi yao, Kibaha Mji imetoa ufafanuzi wa kinachoendelea.

Innocent Byarugaba, ambaye ni Afisa Mawasiliano wa Halmashauri ya Kibaha anajibu hoja za Mdau huyo ambaye alidai kuwa licha ya kuwa wao wapo Kibaha Vijijini lakini wamekuwa wakisumbuliwa na Maafisa wa Kibaha Mji.

Malalamiko ya Mdau soma hapa ~ Maafisa wa Kibaha Mji wanatumia Mgambo na Askari mwenye bastola kututisha ili watuondoe katika Makazi yetu

Byarugaba anaelezea:
Matuga haipo Kibaha Mjini, sisi hatuhusiani na ugomvi wa huko, pili ni kweli kuna maafisa wetu walipigwa picha wakiwa na gari la ofisi yetu walipoenda eneo hilo.

Kwenye hilo eneo kuna sehemu mbili, kipande ni eneo la Kibaha Mjini na Kipande.

Eneo ambalo linamilikiwa na Abdulkadir kuna eneo ambalo lipo Mtaa wa Zegereni zaidi ya Ekari 250, sasa mzee anayeonekana kwenye picha kwa mbele ni Mkuu wa Idara ya Mifugo, Uvuvi na Kilimo sio mpima ardhi ila na yeye ana kiwanja chake maeneo ya Visiga.
Kibaha Viji (1).jpg

Maafisa wa Kibaha Mji.
Kiba (1).jpg

Gari la Kibaha Mji lililopigwa picha na Wananchi maeneo ya Matuga.
Kilichokuwa kinafanyika kwenye picha hiyo ambayo inasambaa mitandaoni ikiwaonesha Maafisa wetu eneo hilo, ni kuwa Afisa wetu mmoja alienda kuonesha eneo analolimiliki kihalali upande wa Kibaha Mjini.

Siku hiyo alienda kuonyeshwa eneo ambalo amelinunua kihalali, mwingine anayeonekana kwenye picha alikuwa na vifaa vya kutambua mipaka, kwa kuwa lile eneo limepimwa siku nyingi na tumetoka kwenye mvua, majani yamekuwa mengi, hivyo vifaa alivyokuwa navyo vinasaidia kumuonesha mipaka ilipo.

Kuhusu wao kutumia gari la ofisi, Wakuu wa Idara na vitengo wanaruhusiwa kutembelea magari ya ofisi.

Kuhusu Wananchi hao kwenda kulalamika hadi kwa Mkuu wa Wilaya ijulikane kuwa DC ana Kibaha Vijijini na Mjini, hivyo kwenda kulalamika kwake ni halali yao (Wananchi wa Matug) kwa kuwa kiongozi huyo ndio mwakilishi wa Rais ngazi ya Wilaya.

Hivyo, walioenda kulalamika walitimiza wajibu wao kwa uhalali na ni haki yao.

Itambulike kuwa shamba au eneo linalozungumzwa ni la mtu binafsi na Halmashauri haihusiki kwa aina yoyote.
IMG_20240706_113437_060 (1).jpg

Wananchi wa Matuga wanaolalamika maeneo yao kuvamiwa na Maafisa wa Kibaha Mji.
 
Wachumia tumbo na wasaka fursa wakitetea matumbo yao. Hakuna cha kujitetea wala kuthibitisha kama kila kitu kiko wazi. Utajitetea vipi chini ya umati wa mashahidi. Sheria ifuate mkondo wake effective immediately.

Waliohusika watolewe mfano mbele ya kadamnasi ili waliobaki wajifunze.
 
Hawana tofauti na wale maafisa waliovamia nyumba ya mtu usiku mnene bila kumuhusisha mtendaji au balozi wakapigwa mishale wakafa.
 
Kama hii kesi isiposhughulikiwa na kumalizika kwa kufuata Sheria na Haki za Kibinadamu. Basi huo utakuwa uthibitisho tosha kwa wananchi kwamba Taifa limekosa sauti moja na limepoteza muelekeo. Kwani hata Serikali itakuwa imewageukia.

Hichi kitu kinatia hasira, na hasira ikikaa sana, huchacha na kuripuka. Na kinachobaki ni mvurugano. Chaos.

Desperation leads to Chaos in Hopes of Salvation.
 
Hakuna halmashauri mbovu Kama kibaha mjini.
1. Wamelazimisha daladala kwenda kupoteza muda Loliondo lakini hawaangalii hiyo barabara.
Eneo hiyo barabara inapoungana na morogoro road karibu na ofisi za DAWASA Ni eneo hatarishi sana, inashangaza kuona hakuna mtendaji anayeliona hili, wao wamengangania magari yaende Loliondo kwenye biashara zao. Hiyo sehemu zinapoungana na Moro road Ni mashimo tu hakuna lami Wala kokoto.
2. Ingependeza daladala zikapitia tumbi kwenye hospitali ili watu wakawaone wagonjwa, kuwapelekea chakula na wagonjwa waondokane na kukodi Bajaj za hao watendaji wa halmashauri ili wafuate tiba Tumbi.
3. Stendi walijenga chini ya viwango, mnakumbuka hata rais alugoma kuifungua Mara ya kwanza, Sasa hivi imefunuliwa Tena kwa kutumia Kodi za wanànchi.
4. Kuna soko wamejenga hapo karibu na stendi kuu sijui Ni kwanini bado halifunguliwi.
5. Tuondoleeni kero ya magari yote kwenda Loliondo. Kwanini iziazishwe ruti za Mbezi Loliondo kwa wanaopenda? Mbona zipo Kama Boko mnemela?
Tunapoteza man hours nyingi Sana kwenda kutizama Loliondo na kuhayarisha maisha tinaporejea Moro Rd kwa faida ya wachache.
6. Kero ya foleni ya Maili moja Hadi Mlandizi sijui Kama Kuna mkubwa hapo kibaha anaiona. Kwanini Ile barabara ya zamani irekebishwe au angalau mashimo yafukiwe tuwe na alternative. Ikitokea ajali au lorry kuharibika barabarani foleni yake sio ya nchi hii.
Nadhani bado Pwani Kuna mkuu wa mkoa, mkuu wa wilaya Kibaha na Kama sikosei kibaha Kuna mkurugenzi.
Hebu watatue kero zetu Basi.
 
Back
Top Bottom