Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 3,984
- 13,760
Mbunge wa Jimbo la Kibaha Mjini, Silvestry Francis Koka aliyekuwa Mgeni rasmi ametoa rai kwa Wananchi na wawekezaji wote kulipa Kodi stahiki kwa wakati kwani fedha hizo Sasa wanashuhudia zikirudi kwenye Jamii kwenda kuondoa kero kwa watoto wetu wanaosoma shule za Msingi na Sekondari za Serikali huku akikemea vikali kuziita shule za Kayumba kutokana na uwekezaji mkubwa unaowekwa na Serikali.
Aidha,Dkt.Shemwelekwa ameongeza kuwa Halmashauri ya Mji Kibaha imepokea Shilingi 5,179,017,622 kwa ajili ya kugharamia Elimu bila Malipo na kutoa rai kwa wadau wa Sekta ya Elimu kuunga mkono jitihada za Serikali kwenye Sekta hii muhimu kwa ajili ya kuandaa Wataalam watakaolitumikia Taifa baadaye
Mkuu wa Wilaya ya Kibaha Mhe.Nikkson Simon John pamoja na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji Kibaha Mhe.Mussa Abdallah Ndomba wamempongeza Mhe.Dkt.Samia Suluhu Hassan,Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuendelea kutoa fedha nyingi kuimarisha Sekta ya Elimu.
Kwa upande wao Swaumu Bakari na Margreth Chuwa kwa niaba ya Wanafunzi wamemshukuru Rais Samia kwa kuendelea kuwajali kwenye sekta ya Elimu na kuahidi kusoma kwa bidii hasa Masomo ya Sayansi.
Halmashauri ya Mji Kibaha yenye jumla ya Wanafunzi 17,424 ina shule 66 za Serikali kati yake za Msingi ni 46 na Sekondari 20.