kibabu mtoto
Member
- Nov 30, 2024
- 64
- 102
Habari Wadai,
Mimi naomba nende Moja Kwa Moja ktk mada yangu, Kuna hii kero ya walimu wilaya kilwa mkoani Lindi kucheleweshewa kulipwa nauli zao za likizo Kwa wakati, inafikia hatua hadi mwalimu husika anaacha kudai nauli yake ya likizo Kwa urasimu uliopo. Kwa mfano, Kuna walimu kadhaa idara ya sekondari hapa halmashauri ya kilwa hawajalipwa nauli zao za likizo tangu walipoenda likizo June na December 2021.
Hali hii ni mwendelezo tu wa yanayotokea halmashauri ya kilwa. Inafikia wakati wakijisika kulipa basi anaweza kulipwa wa aliyeenda likizo hivi karibuni na kuacha wengine hali inayotia doa wilaya hii. Pia, Kwa mfano Mimi nilienda likizo 2022, lakini hadi sasa sikalipwa chochote na sijui nitalipwa lini, siko pekee yangu ila nawakilisha kundi kubwa la wenzangu.
Pia kuhusu kero ya upandishaji madaraja nalo kiasi Fulani ni tatizo, ukimuilza katibu Tsc wilaya majibu anayokupa utatamani usingeuliza, ana tabia ya kuwafokea walimu utadhani anaongea na watoto wake. Acha dharau hii na kujiona, bila walimu usingekuwepo hapo ulipo, wengine tumekuzidi umri halafu unatupanda kichwani.
Naomba hizi kero zitatuliwe kwani hata hayati magufuli aliwahi kusema mtumishi asiende likizo isipokiwa awe amelipwa nauli yake ya likizo.
Nawasilisha.