Halmashauri ya Longido yaipa familia ya Rostam Aziz mapori 3 kwa uwekezaji wa Carbon credit kwa miaka 15

Halmashauri ya Longido yaipa familia ya Rostam Aziz mapori 3 kwa uwekezaji wa Carbon credit kwa miaka 15

Halmashauri ya Longido imeipa familia ya Rostam Aziz mapori 3 kwa uwekezaji wa Carbon credit wa miaka 15 kwa malipo ya Tsh. Milioni 10 kwa kila pori kwa mwaka.

Mkataba huo umesaniwa na Akram Azizi ambaye ni Director wa kampuni iliyoingia mkataba huo ya Kilombero North Safaris.

Marejeo na maboresho ya mkataba huu yatafanyika kila baada ya miaka 5 ili kuendana na mahitaji ya wakati huo.
Mbali na mil. 10 itakayolipwa kwa kila pori, halmashauri ya Longido itanufaikaje tena?
 
Ohoo. Nimejaribu kupitia explanation for dummies kwa haraka, kumbe siyo kama Rostam atavuna kipato bali njia ya ku-contribute kwenye upunguzaji wa uchafuzi wa mazingira.
Rostam huyu huyu aliyeshindwa kuwapa misaada jimboni kwake igunga leo ajafanye charity job longido?
 
Kama kawaida mimbulula ya kibongo, tunauzwa sijui wanatupiga
Kama huna millioni 30 kwa mwaka kwa miaka 15 = millioni 450
Funga domo lako, na kama unayo nenda na wewe ukawekeze,
Budget ya TFS na NEMC kwa mwaka ni zaidi ya billion 100 hiyo tsh milllion kumi si ni sawa na kikombe cha chai baharini kwenye gharama za kutunza.

Huyo Akram atakuwa analinda yeye hiyo misitu au hiyo kazi bado itabaki chini ya TFS na NEMC, halafu yeye shughuli yake ni kwenda kufanya trade offs huko na wazungu na kuvuna mamillioni ya dollar kila mwaka.

Hiyo shughuli ya kuvuna hizo hela si hata TFS wenyewe wanaiweza kama ni kufanya carbon trade tu maana kazi ngumu ya upkeep wanafanya wao tayari.
 
Rostam huyu huyu aliyeshindwa kuwapa misaada jimboni kwake igunga leo ajafanye charity job longido?
Mkuu hii siyo charity per se. Makampuni na viwanda vikubwa vinalazimika kufanya hili ili kuonyesha kuwa wanajali utunzaji wa mazingira. Kwa hiyo nadhani kuwa kampuni yoyote inapofanya hivyo, kuna benefits inapata kwenye ufanyaji biashara wake.
 
Back
Top Bottom