Halmashauri ya Longido yaipa familia ya Rostam Aziz mapori 3 kwa uwekezaji wa Carbon credit kwa miaka 15

Halmashauri ya Longido yaipa familia ya Rostam Aziz mapori 3 kwa uwekezaji wa Carbon credit kwa miaka 15

Mbali na mil. 10 itakayolipwa kwa kila pori, halmashauri ya Longido itanufaikaje tena?
Kwani saizi inavyoyamiliki inanufaikaje? 51% ya Tzn ni mapori ni wewe tuu chagua pori uwekeze.

Tena waje Waarabu wanalipa.hela nzuri kuliko Hawa kina Rostam.

Upumbavu wa kijinga ndio huu ambao Lisu aliwapiga porojo waarabu wamenunua mapori
 
Huyu Akram anafanya hunting miaka mingi na nafikiri ana vitalu vingi vya kuwinda, kuwinda hawa ndugu zetu sehemu ya maisha yao miaka nenda rudi.

Sisi WaAfrica nani anafanya hii biashara zaidi ya kufungia pub, bar, clubs, hotels na apartments, wenzetu wanafanya biashara za dollar na watu wenye uchumi mkubwa, wanaweza kusafisha hela watakavyo kupitia makampuni Yao yaliyopo dubai, London na huku Tanzania.
 
Wote humu mnaweza kutengeneza pesa through carbon credits market, sasa educate yourself how the market works and pay sio kugombana na kulaumu tuu, pesa ipo na hata kama hamna ardhi mnaweza kuwa madalali kama Rostam alivyofanya, nimeangalia kwa haraka per acre market averages 10-16$, kazi kwenu
 
Watasema kwa sababu TFS awawezi hiyo shughuli ni Rostam Aziz na waarabu pekee ndio wanajua sana kutunza misitu na kufanya ‘Carbon trade’.

Bado meli tu ya kuja kutubeba ghalfa watanzania tushauzwa kama vibarua nchi za kiarabu, bila ya sisi wenyewe kujua.
Meli ya nini mkuu, wakati tunatakiwa kuwa vibarua tukiwa hapahapa tunapopaita kwetu kwa jina tu basi!

Kutubeba na kutupeleka huko kwao kunaleta picha mbaya, ile ya enzi za utumwa. Sasa tunafanywa watumwa tukiwa hapa hapa; huku tukijidai sisi ni nchi huru!
 
Wote humu mnaweza kutengeneza pesa through carbon credits market, sasa educate yourself how the market works and pay sio kugombana na kulaumu tuu, pesa ipo na hata kama hamna ardhi mnaweza kuwa madalali kama Rostam alivyofanya, nimeangalia kwa haraka per acre market averages 10-16$, kazi kwenu
Umeandika vyema, ila sikubaliani na lawama unazotutwisha.
Kazi yoyote ni kuwa na uelewa nayo, na pa kuanzia ni jukumu la viongozi kujuwa fursa zilipo na kuwapa uwezo na motisha wananchi wake wazifanye kazi hizo.
Mtu huwezi kujua kitu bila kujuwa kitu hicho kipo, na viongozi wetu wapo pale kutuongoza katika yote haya.

Sasa kwa mfano, chukulia hili la Halmashauri ya Longido. Wilaya nzima ile hakuna watu, kundi au ushirika wa watu wanaoweza kujielimisha na kuifanya kazi hiyo kwa ufanisi?
 
Halmashauri ya Longido imeipa familia ya Rostam Aziz mapori 3 kwa uwekezaji wa Carbon credit wa miaka 15 kwa malipo ya Tsh. Milioni 10 kwa kila pori kwa mwaka.

Mkataba huo umesaniwa na Akram Azizi ambaye ni Director wa kampuni iliyoingia mkataba huo ya Kilombero North Safaris.

Marejeo na maboresho ya mkataba huu yatafanyika kila baada ya miaka 5 ili kuendana na mahitaji ya wakati huo.
Huenda CCM itafaidika kwa kupata pesa za kampeni chini ya nipe nikupe.
"Akram Aziz, mdogo wake Ristam Aziz, alikabiliwa na kesi ya mashtaka 75 ya uhujumu uchumi kwa kukutwa na nyara za Serikali, silaha za aina mbali mbali na risasi zake". Alipeta huku upande wa pili ukinufaika kwa Chaneli 10 TV.
 
Umeandika vyema, ila sikubaliani na lawama unazotutwisha.
Kazi yoyote ni kuwa na uelewa nayo, na pa kuanzia ni jukumu la viongozi kujuwa fursa zilipo na kuwapa uwezo na motisha wananchi wake wazifanye kazi hizo.
Mtu huwezi kujua kitu bila kujuwa kitu hicho kipo, na viongozi wetu wapo pale kutuongoza katika yote haya.

Sasa kwa mfano, chukulia hili la Halmashauri ya Longido. Wilaya nzima ile hakuna watu, kundi au ushirika wa watu wanaoweza kujielimisha na kuifanya kazi hiyo kwa ufanisi?
Umeeleweka mkuu, lakini maisha especially kwenye yanayohusu pesa usitegemee wakuletee mezani na serikali yetu CCM imekaa kipigaji sana wanapeana insiders tuu, na kiukweli NGOs nyingi tuu zinapiga pesa hapo TZ kwa carbon credit market ila wengi hawajui, mkoa wa Kagera wapo wanalipa mamilioni wakulima, ila one thing for sure watu wakifanya homework yao hii market ipo na pesa zipo
 
Hivi kumbe milioni 10 ni nyingi kiasi hiki, mbona Tabata hiyo pesa hupati hata uchochoro wa kujenga choo?
 
Mbona mkataba hauna shida wakuu. Una faida kwa pande zote mbili, na zaidi ni kwa halmashauri
 
Kuna watu wanacheka kwa kulia
Yaani 10m hii hii ya mshahara mmoja wa nje?
Jamaa wanajua kutu wind up
 
Back
Top Bottom