Responded Halmashauri ya Manispaa ya Kibaha: Watumishi wetu wanaoenda likizo hulipwa stahiki zao

Responded Halmashauri ya Manispaa ya Kibaha: Watumishi wetu wanaoenda likizo hulipwa stahiki zao

DogoWaNjombe

JF-Expert Member
Joined
Feb 7, 2022
Posts
3,284
Reaction score
7,708
Emblem_of_Kibaha.png

TAARIFA KWA UMMA​
Halmashauri ya Manispaa ya Kibaha inapenda kuujulisha umma na wadau wote kuwa taarifa iliyosambazwa kupitia JamiiForums ikidai kuwa watumishi wanaoenda likizo mwezi Juni hawalipwi stahiki zao za likizo kwa kisingizio kwamba watumishi wanaoenda likizo ni wengi, si ya kweli na haina uhalali.

Halmashauri ya Manispaa ya Kibaha imekuwa ikitekeleza taratibu za likizo kwa watumishi wake kwa mujibu wa sheria, kanuni na taratibu za utumishi wa umma. Watumishi wanaoruhusiwa kwenda likizo hulipwa stahiki zao kwa kuzingatia taratibu husika.

Kwa Mwaka wa Fedha 2026/2027, Halmashauri tayari imeruhusu watumishi wake kwenda likizo kwa awamu kuanzia mwezi Julai hadi Desemba, na malipo ya stahiki zao za likizo yamekamilishwa kwa watumishi husika.

Kwa hiyo, madai kwamba watumishi hawalipwi likizo kwa sababu ni wengi hayana ukweli. Taarifa hiyo inaonekana kuwa na lengo la kuupotosha umma, kuichafua taswira ya Halmashauri na kuleta taharuki miongoni mwa watumishi na wananchi, jambo ambalo halikubaliki.

Halmashauri inatoa wito kwa wananchi, watumishi na wadau wote kutokuwa na haraka ya kuamini au kusambaza taarifa ambazo hazijathibitishwa kutoka vyanzo rasmi. Kwa taarifa sahihi kuhusu masuala ya kiutumishi na utekelezaji wa shughuli za Halmashauri, wananchi wanashauriwa kufuatilia taarifa zinazotolewa na Halmashauri kupitia njia rasmi.

Halmashauri ya Manispaa ya Kibaha inaendelea kuwahudumia wananchi kwa kuzingatia uwazi, uwajibikaji, sheria na taratibu, na itaendelea kuchukua hatua stahiki dhidi ya taarifa zinazolenga kupotosha umma.

Imetolewa na:
Halmashauri ya Manispaa ya Kibaha
Kibaha

Pia soma ~ Halmashauri ya Manispaa ya Kibaha, Watumishi hatujalipwa hela za likizo mwaka wa tatu sasa
 
Back
Top Bottom