Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo: Ushuru wa Bajaj Mbezi Stendi ni Tsh. 500 inayoshusha abiria na Tsh. 2,000 kwa siku

Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo: Ushuru wa Bajaj Mbezi Stendi ni Tsh. 500 inayoshusha abiria na Tsh. 2,000 kwa siku

BigTall

JF-Expert Member
Joined
Mar 9, 2022
Posts
706
Reaction score
1,716
TAARIFA KWA UMMA@jamiiforums (1).jpg

TAARIFA KWA UMMA
UFAFANUZI WA USHURU WA BAJAJI KATIKA KITUO CHA MABASI CHA MAGUFULI
​

Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo inapenda kutoa ufafanuzi kwa umma kwamba viwango vya ushuru vinavyotozwa kwa bajaji katika Kituo cha Mabasi cha Magufuli vinatofautiana kulingana na aina ya huduma inayofanyika, kama ifuatavyo:

Bajaji inayoshusha abiria wakati wa kutoka katika kituo inatozwa ushuru wa shilingi 500.

Bajaji iliyosajiliwa kituoni inayopakia abiria katika kituo inatozwa ushuru wa shilingi 2,000 kwa siku nzima.

Kwa msingi huo, Halmashauri inawafahamisha waendesha bajaji na wananchi kwa ujumla kuwa shilingi 500 ni ushuru wa bajaji inayoshusha abiria wakati wa kutoka kituoni, wakati shilingi 2,000 ni ushuru wa bajaji inayopakia abiria katika kituo.

Halmashauri inasisitiza kuwa kila malipo yanayofanyika yanapaswa kuambatana na risiti halali inayoonesha kiasi halisi kilicholipwa, kwa mujibu wa taratibu za ukusanyaji wa mapato ya Serikali.

Endapo mwendesha bajaji atatozwa kiasi ambacho hakilingani na kiwango kinachotakiwa au akapewa risiti yenye kiasi tofauti na fedha alizolipa, anapaswa kutoa taarifa kwa Halmashauri kupitia mamlaka husika ili suala hilo liweze kufanyiwa uchunguzi na hatua stahiki zichukuliwe.

Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo inaendelea kusimamia kwa karibu ukusanyaji wa mapato katika maeneo yake na inasisitiza uwazi, uwajibikaji, uadilifu na uzingatiaji wa taratibu za Serikali katika utoaji wa huduma na ukusanyaji wa mapato.

Aidha, Halmashauri inawataka waendesha bajaji na wananchi kwa ujumla kushirikiana na Serikali kwa kutoa taarifa kuhusu ukiukwaji wowote wa taratibu za ukusanyaji wa mapato ili hatua stahiki ziweze kuchukuliwa.

Imetolewa na:
KITENGO CHA MAWASILIANO SERIKALINI
HALMASHAURI YA MANISPAA YA UBUNGO



Pia soma ~ Stendi ya Magufuli, Bajaj wanaombwa Sh 1,000 ila wanapewa risiti ya Sh 500, anayegoma anapewa risiti ya Sh 2,000
 
Hii issue ya risiti ya Tsh. 2,000 kwa anayegoma ni ubabe wa kijinga.
 
Ndio maana mnalazimisha wote kushukia hapo ili mdake hizo elf 2
 
Back
Top Bottom