KERO Halmashauri ya Masasi – Mtwara haijawalipa Watendaji wa Vijiji waliosimamishwa kazi tangu Awamu ya 5

KERO Halmashauri ya Masasi – Mtwara haijawalipa Watendaji wa Vijiji waliosimamishwa kazi tangu Awamu ya 5

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
A

Anonymous

Guest
Halmashauri ya Wilaya ya Masasi Mkoani Mtwara haijawalipa Watendaji wa Vijiji waliosimamishwa kazi kipindi cha Serikali ya Awamu ya 5 kutokana na suala la vigezo vya elimu.

Tumefanya jitihada kuwasiliana na Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo kwa njia ya WhatsApp lakini hajajibu badala yake amedai yupo likizo.

Watendaji hao wanalalamika kuitwa kujaza fomu na barua ya madai kila baada ya miezi kadhaa lakini hawalipwi, sasa ni zaidi ya miaka 6 imepita.

Waziri Mkuu mstaafu mh. Kassim Majaliwa alitoa maagizo mara kadhaa wale Watendaji walipwe lakini hawakulipwa na wakapuuzwa.

Hili naomba liwafikie kwasababu Watendaji wengine wamefariki na familia zao hazielewi pa kuanzia.

Wengine wameshastaafu walikata tamaa wakaona hawawezi kupata tena stahiki zao.

Serikali iwasaidie hawao Watendaji, wengi wao ni watu wazima na wengine ni wazee, hicho kiasi kidogo wanachodai wangepewa ili wawe na amani, kwani kuwanyima ni mwanzo wa kuwafanya watendaji wengine pia washindwe kuwa ‘active’ na kutokuwa na uzalendo wakijua nao pia ipo siku watafanyiwa hayohayo.
 
Moja ya halmashauri zinazoendesha mambo yake kizembe na hovyo sana
 
Back
Top Bottom