Influenza
JF-Expert Member
- Jul 1, 2018
- 1,509
- 3,756
Hayo yamebainishwa katika taarifa iliyowekwa na TAMISEMI katika ukurasa wao wa Mtandao wa X
Pia soma LGE2024 - Simiyu: Karatasi za kupigia Kura zakamatwa zikiwa zimewekewa tiki kwa wagombea wa CCM
TAARIFA KWA UMMA JUU YA UPOTOSHAJI WA UWEPO NA KARATASI FEKI(BALLOTPAPER) ZA KUPIGIA KURA KATIKA HALMASHAURI YA MJI BARIADI
Msimamizi wa Uchaguzi Halmashauri ya Mji Bariadi Ndugu. Adrian Jungu anapenda kuutaarifu umma kupuuzia taarifa za uwongo za uwepo wa karatasi feki(ballotpaper)za kupigia kura katika baadhi ya maeneo ndani ya Halmashauri ya Mji Bariadi ambapo taarifa hizo sio sahihi na zinalenga kuleta taharuki na kuchafua taswira ya zoezi zima la Uchaguzi katika Mji wa Bariadi.
Kwa mujibu wa mtoa taarifa hizo zimedai kuwa karatasi za uchaguzi wa Serikali za Mitaa zimetolewa siku ya Jana Novemba 26 hali ambayo sio kweli kwani uhalisia wa zoezi la ugawaji ugawaji wa karatasi za kupigia kura limefganyika leo Novemba 27 alfajiri katika maeneo yote ya vituo vya Kupigia Kura.
Aidha Msimamizi wa Uchaguzi Halmashauri ya Mji Bariadi anapenda kuwatoa hofu wananchi wote na kuwataka kuendelea kujitokeza kwa wingi katika zoezi la kupiga kura ambalo linaendelea katika vituo vyote.
Hata hivyo karatasi zote ambazo zimeonekana kuwa ni feki zipo chini ya vyombo vya Ulinzi na Usalama kwa ajili ya uchunguzi wa karatasi hizo na pindi uchunguzi ukikamilika taarifa itatolewa.

Adrian J. Jungu
MSIMAMIZI WA UCHAGUZI HALMASHAURI YA MJI BARIADI