Halmashauri ya Mji Kibaha kutoa mikopo ya Tsh. Bilioni 1.6 kwa Vikundi vya Wanawake, Vijana na Watu wenye ulemavu

Halmashauri ya Mji Kibaha kutoa mikopo ya Tsh. Bilioni 1.6 kwa Vikundi vya Wanawake, Vijana na Watu wenye ulemavu

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
3,984
Reaction score
13,760
Halmashauri ya Mji Kibaha inatarajia kutoa mikopo kwa Vikundi vya Wanawake, Vijana na Watu wenye ulemavu yenye thamani ya Shilingi 1,169,428,549 ili kuwawezesha kupambana na adui umasikini

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Kibaha Dkt.Rogers Jacob Shemwelekwa ametangaza uwepo wa fedha hiyo kwa ajili ya kuvikopesha vikundi vyenye sifa na kwamba fedha hiyo imetengwa katika robo ya pili ya Mwaka wa fedha 2024/2025

Mkuu wa Divisheni ya Maendeleo ya Jamii wa Halmashauri ya Mji Kibaha Leah Lwanji amebainisha sifa za vikundi vitakavyokidhi vigezo vya kukopeshwa kuwa ni kikundi kilichotambuliwa rasmi na kupewa cheti na Halmashauri,kikundi kinachojishughulisha na ujasiliamali mdogo au kati pamoja na kinachotarajia kianzisha ujasiliamali.

Aidha,Lwanji ameongeza kuwa kikundi cha wanawake na Vijana kiwe na watu wasiopungua watano (5) huku kikundi cha watu wenye ulemavu wasipungue wawili (2)

Kwa upande Mwingine Leah Lwanji amesema waombaji wanapaswa kuwa na barua ya kikundi iliyopitishwa na Mtendaji wa Kata, Muhtasari wa kikundi wa Kuomba Mkopo,andiko rahisi la Mradi unaoombewa Mkopo pamoja na namba ama kitambulisho cha Taifa

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Kibaha Dkt.Rogers Jacob Shemwelekwa ametoa rai kwa makundi yote yenye sifa Kuomba mikopo hiyo ili kutimiza malengo ya Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Dkt.Samia Suluhu Hassan ya kutokomeza umaskini sanjali na kuboresha maisha ya Watanzania.
 
Back
Top Bottom