Wanajua kiongozi wao Hana habari Wala hajui kinachoendelea,utakuta kumepelekwa zaidi ya mil 400 hapo na wajanja wametafuna.wale kwa urefu hamna namna
Kuna muda ni ngumu sana kwa Tanzania.
Unaweza kuwa sahihi,Raisi akapeleka 400M,lakini je tunataka Rais afuatilie kila jambo?
Wizara husukia ina Waziri,Naibu(2),Katibu,chini yao kuna Maafisa kibao ...mkoa una Mkuu wa mkoa ambaye wanajinadi ni Rais wa Mkoa,kuna Mkuu wa Wilaya,Afisa Elimu Mkoa,Wilaya,Kata.
Mimi nasema kila siku,Watanzania tuna roho mbaya sana hasa baadhi ya viongozi,mfano wa hapo kwenye hiyo Wilaya yenye Shule kama hiyo.
Na ukute hapo walitoa hela ya kumchangia Mama kuchukua fomu.
Nilibahatika kwenda Zanzibar,b4 Mama kuwa raisi na Mwinyi na sasa aisee...kuna kiasi kule watu wapo serious na shule zao.
Juzi hapo imezinduliwa Shule ya Msingi kali sana,na wanasema kwa aiana ya shule zile imetumia 4Billion.
Na zitajengwa nyingi sana kwa mfano ule.
Juzi tu hapa kuna taarifa Shule ya Wasichana Mbeya haijaisha mpaka sasa,Wakati Shule ya wasichana zengine zimekamilika na zipo vyema.
Mama wa watu akiwa mkorofi ataitwa kama ilivyokuwa kwa Baba wa watu Magufuli.
Wachawi ni sisi wenyewe.Tuna mengi ya kuandika hapa...