KERO Halmashauri ya Wilaya Kasulu DC, Walimu tulioajiriwa 2025 hatujathibitishwa kazini

KERO Halmashauri ya Wilaya Kasulu DC, Walimu tulioajiriwa 2025 hatujathibitishwa kazini

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
A

Anonymous

Guest
Walimu tulioajiriwa na Halmashauri ya Wilaya ya Kasulu (Kasulu DC) mwezi Julai 2025 bado hatujathibitishwa kazini hadi sasa.

Hatujapewa maelezo ya wazi kuhusu sababu ya kuchelewa kwa uthibitisho huo, hali ambayo imekuwa ikitutia wasiwasi na kutokuwa na uhakika kuhusu ajira zetu.

Tunaomba Halmashauri ya Wilaya ya Kasulu kulitolea ufafanuzi suala hili na kuchukua hatua stahiki ili walimu tuweze kuthibitishwa kazini kwa wakati.

Tunaomba sauti yetu isikike na suala hili lifanyiwe kazi.
 
Back
Top Bottom