Pre GE2025 Halmashauri ya Wilaya ya Geita imetoa mkopo wa milioni 689 kwa vikundi 39 vinavyoundwa na wanawake, vijana, na watu wenye ulemavu

Pre GE2025 Halmashauri ya Wilaya ya Geita imetoa mkopo wa milioni 689 kwa vikundi 39 vinavyoundwa na wanawake, vijana, na watu wenye ulemavu

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

The Watchman

JF-Expert Member
Joined
Nov 7, 2023
Posts
896
Reaction score
1,427
Halmashauri ya Wilaya ya Geita imetoa mkopo wa asilimia 10 wenye thamani ya shilingi milioni 689 kwa vikundi 39 vinavyoundwa na wanawake, vijana, na watu wenye ulemavu. Mkopo huo unalenga kuwawezesha wanufaika kukuza shughuli zao za kiuchumi na kujitegemea, ikiwa ni sehemu ya juhudi za serikali kuinua maendeleo ya makundi maalum ndani ya jamii.

Akizungumza wakati wa hafla ya utoaji wa mikopo hiyo, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo, Karia Rajabu Magaro, alisema kuwa halmashauri imeendelea kutoa mikopo kwa makundi hayo, huku kiasi cha shilingi bilioni 1.2 kikiwa kimetengwa kwa ajili ya awamu nyingine ya utoaji wa mikopo.

Soma pia: Pre GE2025 Special Thread: Mijadala na Matukio ya Uchaguzi Mikoa yote Tanzania Bara na Zanzibar kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025

Kwa upande wake, Mkuu wa Idara ya Maendeleo ya Jamii wa halmashauri hiyo, Jonas Kilave, alifafanua kuwa vikundi vilivyopewa mikopo vilichaguliwa kwa kuzingatia vigezo vilivyowekwa kwa mujibu wa sheria.

Viongozi wa wilaya, akiwemo Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Geita, Charles Kazungu, na Katibu Tawala wa Wilaya ya Geita, Lucy Beda, walieleza umuhimu wa mikopo hiyo katika kuinua uchumi wa wanufaika na jamii kwa ujumla.

Baadhi ya wanufaika wa mkopo huo walionesha furaha yao na kuelezea matarajio yao juu ya maendeleo ya vikundi vyao baada ya kupokea fedha

 
Back
Top Bottom