tripleec
Senior Member
- Oct 19, 2022
- 169
- 159
Nikiwa kama mwananchi nimeona nitumie jukwaa hili maana naamini wahusika wengi wapo humu na wengi wanaweza saidi kupaza sauti.
Nimepita eneo la Sinza kumekucha karibu na kanisa la KKKT kiukweli hali ya usalama wa afya ni mbaya kwa wakazi hao.
Nilifanya mahojiano na baadhi ya wakazi wa maeneo hayo nini kimewasibu wakasema yapata kama miezi 2 gari la kuzoa taka hawajawahi kuliona licha ya kuwa wanalipa pesa ya huduma hiyo.
Nikawauliza je mmeshatembelea ofisi za Serikali ya mtaa majibu niliyopewa ni kuwa mwenyekiti na katibu wamekuwa wakiwapa majibu tofauti mmoja anasema linakuja tangulia mwingine anajibu gari haliji tena.
Nikajiuliza sasa kama hakuna gari kwanini waasitafute tenda nyingine , mwananchi mmoja akanijibu kuwa wameambiwa mpaka tenda ya huyu wa sasa iishe mwakani ndiyo watatafuta mtu mwingine.
Ifike mahala wale wa mikokoteni waachiwe kazi hii maana watu wapo tayari kulipia huduma lakini mzoaji hayupo mwisho wa siku nachelea au naogopa kama wakiamua kuziacha barabarani na hali hii ya mvua ni hatari kwa miundo mbinu lakini npia na magonjwa ya mlipuko.
Nimemabatanisha picha katika moja ya mtaa unaitwa Chuma nyuma ya kanisa la KKKT sizna kumekucha.