Halmashauri ya Wilaya ya Ubungo tusaidieni hili la taka Sinza, hali ni mbaya

Kipindi cha mvua huko dampo pa kutupa taka hakuingiliki

Ova
 
Nipeni tenda nilete magari ya taka
Kabla hamjapata magonjwa hebu jiongezeni kwanza msafishe na kuzoa taka mkazitupe halafu ndio mpaze sauti kila sehemu
 
Hizi picha mbona ni za Lagos Nigeria?
 
Leo niliona nipite tena kwa ndugu zangu wa juzi nione nini kimeendelea naona lalamikomlao limechukuliwa hatua na kama kunamdau humu au muhusika basi nami sina budi kumshukuru kwa kuwaona hawa ndugu zetu na kujali afya zao.Taka zimetolewa na wanasema ilikuja maalum kwa ajili ya eneo hilo. Nimefarijika jukwaa hili kuona hatua imechukuliwa.
 
Kwa Manispaa ya Ubungo takataka ni kila sehemu kwa sasa, hata Mabibo barabara ya ubungo maziwa to kigogo wananchi wameamua kuzirundika barabarani pembezoni mwa mifereji ya maji ya mvua ikitokea mvua kubwa itazisomba na kuziingiza mto msimbazi zote, zipo muda kila tukipita barabara hiyo twazikuta.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…