Halmashauri zinazokusanya kuanzia bilioni 5, zaelekezwa kutenga 10% kuboresha miundombinu ya barabara

JUMA JUMA

JF-Expert Member
Joined
Jan 5, 2013
Posts
790
Reaction score
964
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Mhe. Innocent Bashungwa amewaelekeza Wakurugenzi wa Halmashauri zinazokusanya mapato ya ndani kuanzia bilioni 5 kwa mwaka kuhakikisha wanatoa asilimia 10 kati ya asilimia 60 inayotengwa kutekeleza miradi ya maendeleo kwa ajili ya kuboresha miundombinu ya barabara za lami za mitaa.

Bashungwa ametoa maelekezo hayo leo Septemba 21, 2022 Bungeni jijini Dodoma, wakati akijibu swali la Mhe. Jerry Silaa Mbunge wa Ukonga kuhusu nini kauli ya Serikali juu ya kutenga fedha za mapato ya ndani kwa ajili ya kujenga barabara za lami mitaani katika mkoa Dar es Salaam.

“Nimeshatoa maelekezo kwa halmashauri ambazo zinatenga asilimia 60 ya mapato ya ndani kwa ajili ya miradi ya maendeleo kuhakikisha wanatoa asilimia 10 kwa ajili ya kutengeneza barabara za mitaa ukiwemo mkoa wa Dar es Salaam.”

Bashungwa amezitaka Halmashauri hizo kushirikiana na Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini Tanzania (TARURA), kuweka mpango mkakati wa pamoja kuhakikisha asilimia 10 inayotengwa, inatengeneza barabara ambazo zitaendana na uhalisia wa matumizi ya fedha.

Aidha, Bashungwa amesema serikali inaendelea kufanya mazungumzo na Benki ya Dunia juu ya mkopo wa fedha kwa ajili ya mradi wa uboreshaji wa miundombinu katika Jiji la Dar es Salaam awamu ya pili (DMDP).
IMG-20220921-WA0131(1).jpg
IMG-20220921-WA0132(2).jpg
 
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Mhe. Innocent Bashungwa amewaelekeza Wakurugenzi wa Halmashauri zinazokusanya mapato ya ndani kuanzia bilioni 5 kwa mwaka kuhakikisha wanatoa asilimia 10 kati ya asilimia 60 inayotengwa kutekeleza miradi ya maendeleo kwa ajili ya kuboresha miundombinu ya barabara za lami za mitaa.

Bashungwa ametoa maelekezo hayo leo Septemba 21, 2022 Bungeni jijini Dodoma, wakati akijibu swali la Mhe. Jerry Silaa Mbunge wa Ukonga kuhusu nini kauli ya Serikali juu ya kutenga fedha za mapato ya ndani kwa ajili ya kujenga barabara za lami mitaani katika mkoa Dar es Salaam.

“Nimeshatoa maelekezo kwa halmashauri ambazo zinatenga asilimia 60 ya mapato ya ndani kwa ajili ya miradi ya maendeleo kuhakikisha wanatoa asilimia 10 kwa ajili ya kutengeneza barabara za mitaa ukiwemo mkoa wa Dar es Salaam.”

Bashungwa amezitaka Halmashauri hizo kushirikiana na Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini Tanzania (TARURA), kuweka mpango mkakati wa pamoja kuhakikisha asilimia 10 inayotengwa, inatengeneza barabara ambazo zitaendana na uhalisia wa matumizi ya fedha.

Aidha, Bashungwa amesema serikali inaendelea kufanya mazungumzo na Benki ya Dunia juu ya mkopo wa fedha kwa ajili ya mradi wa uboreshaji wa miundombinu katika Jiji la Dar es Salaam awamu ya pili (DMDP).View attachment 2363923View attachment 2363924
Wazionee hurumu aisee
 
Back
Top Bottom