Halmashauri zitaacha ubadhirifu wa fedha za umma pale wakurugenzi hawatakuwa wasimamizi wa uchaguzi mkuu

Mwanamayu

JF-Expert Member
Joined
May 7, 2010
Posts
11,662
Reaction score
6,888
Kila mwaka hawa wakurugenzi walio wengi wanakutwa na tuhuma za ubadhilifu wa fedha za umma kwenye halmashauri zao.

Swali: jeuri hii wanaipata wapi? Na aliyewateua mbona kama anawagwaya hivi? Nionavyo mimi ni kuwa wakiondolewa kwenye kusimamia uchaguzi mkuu, ndipo tatizo hili litapungua au kuisha kabisa. Au wasiwe wateule wa Rais, waombe hizo kazi na kusailiwa.
 
Ni kweli kabisa,

Na pale ambapo watakapoanza kupatikana Kwa kuomba na usaili na vettig ma sio utaratibu wa sasa wa uteuzi wa kujuana.
 
Hii nchi kila mtu ni 'potential thief' ni suala la kupata fursa ya kuiba tu.

Wanaiba kwa sababu hawana uhakika wa kesho yao. Maana mtu anajua wakati wowote anaweza kutumbuliwa. Na unavyojua jamii zetu wana methali 'ALIYE JUU MNGOJE CHINI' ukitumbuliwa na hukuiba jamii inakucheka.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…