Halotel wanaibia wateja!

Halotel wanaibia wateja!

I am Groot

JF-Expert Member
Joined
Jul 20, 2018
Posts
3,929
Reaction score
10,747
Salaam

Kuna vitu siku hizi sivielewi na huu mtandao. Nimeviona mara kadhaa nikabaki kujiuliza na sina jibu. Unanunua bando la internet ila hawa washenxi wanakula bando lako zaidi ya 30% hujui limeenda wapi.

Kuna watu watakuja kuniambia simu yangu kuna app zinarun kwenye background!. Hili ni HAPANA. Jambo hili nalijua na huwa siruhusu kitu hiko ila taabu iko palepale.

Mfano leo; nilinunua bando la 500 la mb 245. Nikashusha file la mb 111.78 tu. Cha kushangaza ni kwamba eti naambiwa mb nilizobakiwa nazo ni 48 tu. Hizo nyingine wamezipeleka wapi. Hapa hiyo page niliyoingia nimeenda direct kwenye download section b'coz nilishaiandaa kabla. Hakukuwa na Ad ya aina yoyote ile.

Daah kwa nini wafanye hivi tuwalipe bado wanaona wanachotupa kama wametupendelea sana wanachukua bila ruhusan. Jambo hili liangaliwe upya.
 
Makampuni ya simu yamefanya cartel ya kuwanyonya walaji wao.

Huduma zao siku hizi sio za ushindani,yaani utafikiri zote kampuni za mtu mmoja.

Halotel Ni vietel,hii Mkwere and family wanahusika!!

Tigo na Zantel ni Rostam.

Airtel ndio hao hao wakubwa waliibemenda TTCL wakaanzisha Celtel,ikazaa Zaina(Zain) na sasa Airtel.

Waziri kama Nape ni kibaraka wa wakubwa,wanabariki tu uhuni.

Tume ya ushindani nayo imetiwa mfukoni!!
 
Weka firewall Pima na wewe matumizi yako ya internet.

Lets say umetembelea site fulani kudownload file, site ina matangazo ya Video ni mb zako ndio zina load hizo video, unakuta umetembelea page kadhaa za Hio site MB 50 zime kata unalaumu Mitandao inaiba.
 
Jamani nimetoka kuongea na huduma kwa wateja sasa hivi tumebishana hadi nimemtukana.

Nimenunua kifurushi nikiwa offline kuna kazi nilikuwa nafanya baada ya nusu saa nawasha data nikatumiwa meseji 2 ya umetumia 75% na kifurushi kimeisha ndani ya sekunde moja wakati sijafungua chochote bado.

Kabla ya hapo leo hiihii nilinunua kifurushi hata sijatumia sana kikaisha jamani leo halotel wanafanya wizi wa wazi kabisa wa vifurushi.
Ukiwapigia simu wanakwambia tunaona matumizi umetumia, nitatumia vipi na nipo offline??
 
Ahahahahh huu mtandao nao ukaangaliwe

Sent from my itel L5007 using JamiiForums mobile app
 
Weka firewall Pima na wewe matumizi yako ya internet.

Lets say umetembelea site fulani kudownload file, site ina matangazo ya Video ni mb zako ndio zina load hizo video, unakuta umetembelea page kadhaa za Hio site MB 50 zime kata unalaumu Mitandao inaiba.
Screenshot_20230915-153829.jpg

Hapo mbona sioni kilichotumia hizo MB?? Naomba maelekezo mkuu maana sielewi
 
Ndo maana mm wakati mwingine naamua kutumia kitochi maana 🤔🤔
 
Back
Top Bottom