Hama hama ya viongozi wa CHADEMA inarudisha nyuma hamasa ya vijana kuupambania upinzani

Hama hama ya viongozi wa CHADEMA inarudisha nyuma hamasa ya vijana kuupambania upinzani

Siku alipohama Dkt. Slaa, vijana wengi wa CHADEMA walivunjika moyo. Na ndiyo ikawa mwanzo wa kupungua kwa kishindo na nguvu ya maandamano ya CHADEMA.

Hata walipofuata wengine akina Mashinji, Katambi, n.k hakuna aliyestuka tena, maana watu waliwapuuza.

Ni muda umepita sasa, hatujashuhudia hizi hama hama, na ilianza kuaminika kuwa waliobaki ndiyo roho na moyo wa CHADEMA.

Lakini usajili wa leo wa Msigwa ndani ya CCM umetonesha makovu ya donda lililoanza kupona.

Nashawishika kuamini kuwa ipo siku hata Mbowe, Lisu, Mnyika, Heche na Lema watajiunga CCM.

Ni hayo tu!

Soma ===>> Kuelekea 2025 - Aliyekuwa Mwenyekiti wa CHADEMA, Kanda ya Nyasa, Mchungaji Peter Msigwa ahamia CCM
Kama Mdee na Bulaya walienda, me sidhani kama upinzani wanamaanisha wanachokipigania.
 
Kwani Hoa wakina LISU, Mnyika ,Mbowe ndio upinzani? rudu Darasani kasome maana ya upinzania, make inaonekana unawategemea watu sana. Usishangae movement ya kuondoa utawala huu ikaja kuanzishwa hata na Mchoma mkaaa, au Mvuvi,

Mmewekeza sana kwenye watu, na ndio maana wale Gener Z hawataki kusikia hata wakina Raila Odinga.

Sasa endeleeni kuwekeza kwenye mtu badala ya Ideology yenyewe.
Ndo hapo ata mimi nashangaa!! badala ya watu kuchukia mifumo na kuamua kusuka upya system za mihimili yetu ya kiserikali wao wanabaki kushabikia watu na vyama hao wote ni walewale kitakacho weza kuwamanage ni mifumo tutayoichagua ili iwacontrol kwa faida ya nchi.
 
Wakenya kwenye masuala ya kufuatilia miziki, mipira, msambwanda, mtandao bado wako chini mno watanzania wapo bize mno kwenye hizo sekta.
Tazama vizuri takwimu zako, mkuu.
Wakenya wako mbele ya Watz kwenye hayo mambo yote...
 
Back
Top Bottom