Hamas na waisrael wameamua vita sasa basi.Netanyahu akilazimisha hatakuwa na pa kutokea.

Hamas na waisrael wameamua vita sasa basi.Netanyahu akilazimisha hatakuwa na pa kutokea.

Webabu

JF-Expert Member
Joined
Apr 29, 2010
Posts
10,509
Reaction score
16,734
Taarifa za karibuni kabisa zinaeleza kuwa makundi ya wapiganaji huko Gaza wakiongozwa na Hamas wamesema wamekubaliana na mpango wa kumaliza vita vya miaka miwili kati yao na Israel.

Hatua hiyo imekuja kufuatia mazungumzo yaliyokuwa yakiendelea nchini Misri yakisimamiwa na Qattar na Misri yenyewe ambayo yamehusisha mapendekezo ya Steve Witkoff mwakilishi wa raisi Trump yaliyowasilisha mwezi July.

Chini ya makubaliano hayo Hamas wamekubali kusitishwa vita kwa siku 60 na wao kuachia huru mateka nusu kati ya waliobaki nao.Pamoja na hivyo jeshi la Israel lijiondoe maeneo muhimu ya Gaza kuruhusu misaada kuingia jimboni humo bila vikwazo.

Matamko hayo ya makundi ya wapalestina yamekuja wakati nyeti katika maamuzi ya waziri mkuu Benjamini Netanyahu na baraza lake linaloongoza vita hivyo.Huku viongozi hao wakikusudia kupeleka majeshi zaidi ya laki moja Gaza kwa kile wanachokiita kukamilisha kazi yao ya kubomoa miundombinu yote ya Hamas.Wanachi wa Israel kwa wingi wamesema wanataka vita hivyo visitishwe mara moja.

Wananchi wa Israel wanasema hawaoni sababu ya wapalestina kuhamishwa tena kupelekwa kusini ya jimbo hilo na wala jeshi kuingia huko kwa usalama wa mateka waliobaki pamoja na askari watakaoshiriki hatua hiyo ya vita.

Taarifa za ndani zilizofichuliwa na waandishi wa habari zimebainisha kuwa Netanyahu na baraza lake
wamedhamiria kuendelea na kuiteka Gaza yote lakini wataalamu na viongozi wa kijeshi wastaafu wamesema kwa sasa jeshi la IDF halina askari wa kutosha wa kufanya kazi hiyo na moyo wa kupigana wa askari waliopo uko chini sana huku wakihofia kukumbana na upinzani mkali kutoka kwa wapiganaji wa Hamas waliojificha kwenye vifusi.

Kumaliza vita na kutangaza kuwashinda Hamas pamoja na kuwapata mateka ndio karata pekee iliyobaki kwa uhai wa maisha ya kisiasa ya Benjamini Netanyahu katika muda ambao uchaguzi umekaribia sana.

Kuchoshwa na vita visivyokuwa na sababu hakupo Palestina na Israel peke yake bali pia huko Marekani,Ukraine na Urusi.Raisi Trump wa Marekani kwa sasa yupo kwenye juhudi kubwa za kumaliza vita vya miaka mitatu baina ya Ukraine na Urusi ambavyo serikali yake ilikuwa upande wa Ukraine.
 
Vita haviwezi kwisha mpaka magaidi wote waangamizwe kabisa kwa sababu wenyewe ndio walianzisha hivyo vita.
 
Vita haviwezi kwisha mpaka magaidi wote waangamizwe kabisa kwa sababu wenyewe ndio walianzisha hivyo vita.
Umekaa kwa Sada yako unaandika tu utumbo. We hivi vita vinakusaidia nini? Hakuna umuhimu wa vita na watu kuuana bila sababu.
 
Back
Top Bottom