Hamas Wajuta wanasema wangujua haya matokeo dhidi ya Israel wasingevamia October 7th

Hamas Wajuta wanasema wangujua haya matokeo dhidi ya Israel wasingevamia October 7th

Mlaleo

JF-Expert Member
Joined
Oct 11, 2011
Posts
14,809
Reaction score
11,825
Hamas politburo member Moussa Abu Marzouk, front, attends the funeral of Saleh Arouri, in Beirut, Lebanon, January 4, 2024. (AP Photo/Hussein Malla)
Moussa Abu Marzouk, mbele, anahudhuria mazishi ya Saleh Arouri, huko Beirut, Lebanon, Januari 4, 2024. (Picha ya AP/Hussein Malla)

Kiongozi wa juu wa chama cha kisiasa za kigaidi cha Hamas Moussa Abu Marzouk alisema hangeunga mkono uvamizi na mashambulizi ya Oktoba 7, 2023 kusini mwa Israel ikiwa angejua matokeo yatakuwaje kwa Ukanda wa Gaza, katika mahojiano na The New York Times ambayo yalifanywa Ijumaa na kuchapishwa Jumatatu.

Shambulio la Oktoba 7 - ambapo maelfu ya magaidi wanaoongozwa na Hamas walivamia mpaka wa Gaza na Israel, na kuua takriban watu 1,200, wengi wao wakiwa raia, na kuchukua mateka 251, huku kukiwa na kukithiri kwa vitendo vya ukatili na unyanyasaji wa kijinsia - liliibua vita vilivyofuata huko Gaza, ambavyo vimesababisha uharibifu mkubwa kwa maelfu ya watu waliouawa Kitendo kilichosababisha Raisi wa Marekani Trump kuamua kuichukua Gaza na kuwahamisha raia wote Gaza zaidi ya milion 2 bila kurejeshwa tena katika Ukanda huo.

"Kama ilitarajiwa kwamba kilichotokea kingetokea, kusingekuwa na Oktoba 7," Abu Marzouk alisema, akisisitiza kwamba - ingawa alidai kuwa hakujua maelezo kamili ya shambulio lililopangwa - hangeweza kujileta kuidhinisha, akijua anachojua sasa.

Kauli hiyo ya majuto iliashiria kuondoka kwa kauli za awali za viongozi wa Hamas. Wiki chache baada ya uvamizi huo, kwa mfano, mjumbe wa politburo Ghazi Hamad alitangaza hadharani kwamba Oktoba 7 ilikuwa "mara ya kwanza tu, na kutakuwa na ya pili, ya tatu, ya nne," akisema, "tuko tayari kulipa" bei, na kuapa kuendelea hadi Israeli itakapoangamizwa kabisa.

Katika wiki kadhaa tangu kufikiwa kwa makubaliano ya kuachiliwa huru kwa mateka ya kusitisha mapigano mwezi uliopita, Hamas na washirika wake pia mara kwa mara wameviita vita hivyo kuwa ni "ushindi" kwa sababu yao.

1740596856447.png

Wapalestina wanaishi kati ya vifusi vya nyumba zao, zilizoharibiwa katika vita kati ya Israel na Hamas, katika mji wa Khan Younis, kusini mwa Ukanda wa Gaza, Februari 23, 2025. (Abed Rahim Khatib/Flash90)

Kwa hakika, matamshi ya Abu Marzouk yalipingwa haraka na msemaji wa Hamas Hazem Qassem, ambaye alisema: "Tabia ya uchokozi na ya uharibifu ya uvamizi huo ndiyo sababu ya uharibifu huko Gaza. Epic ya Oktoba 7 inaashiria mabadiliko ya kimkakati katika mapambano ya kitaifa ya Palestina.

Katika taarifa iliyotolewa muda mfupi baadaye na kundi lenyewe, Hamas ilidai kuwa maoni ya Abu Marzouk hayakuwa "sahihi na yametolewa nje ya muktadha."

"Mahojiano hayo yalifanyika siku chache zilizopita na taarifa zilizochapishwa hazikuonyesha maudhui kamili ya majibu," kundi hilo la kigaidi lilidai.

Katika mahojiano hayo, Abu Marzouk alisema kunusurika kwa Hamas, licha ya kampeni ya Israel huko Gaza, ni "aina ya ushindi." Alilinganisha kundi la kigaidi, ambalo limekuwa serikali kuu ya Gaza tangu kuliondoa kundi kuu la Mamlaka ya Palestina la Fatah katika mapinduzi ya 2007, na mtu wa kawaida ambaye amenusurika kwenye mechi ya ndondi na bingwa wa uzito wa juu Mike Tyson. Lakini alisema kuwa kwa maneno kamili, itakuwa "haikubaliki" kuita vita kuwa ushindi kwa kundi la kigaidi.

"Tunazungumza kuhusu chama [Israeli] ambacho kilipoteza udhibiti na kulipiza kisasi dhidi ya kila kitu," Abu Marzouk alidai. "Huo sio ushindi kwa hali yoyote."

===================
Senior Hamas politburo member Moussa Abu Marzouk said he would not have backed the October 7, 2023, invasion and onslaught in southern Israel if he had known what the consequences would be for the Gaza Strip, in an interview with The New York Times that was conducted on Friday and published on Monday.

The October 7 attack — in which thousands of Hamas-led terrorists burst across the Gaza-Israel border, killing some 1,200 people, mostly civilians, and taking 251 hostages, amid rampant acts of brutality and sexual assault — sparked the subsequent war in Gaza, which has devastated the enclave, seen tens of thousands killed, and prompted the US president to call for the forced relocation of the more than 2 million residents of the Strip.
January 4, 2024. (AP Photo/Hussein Malla)

The war has also, through fighting on other fronts, significantly weakened Iran’s so-called “Axis of Resistance,” devastating the Hezbollah terror group in Lebanon, and indirectly contributing to the collapse of the Iran-backed Bashar al-Assad regime in Syria.

“If it was expected that what happened would happen, there wouldn’t have been October 7,” Abu Marzouk said, asserting that — though he claimed to not have been privy to the exact details of the planned assault — he could not have brought himself to approve it, knowing what he knows now.
The statement of regret marked a departure from previous statements by Hamas officials. A few weeks after the invasion, for example, politburo member Ghazi Hamad publicly declared that October 7 was “just the first time, and there will be a second, a third, a fourth,” saying, “we are ready to pay” the price, and vowing to continue until Israel was totally annihilated.

In the weeks since a hostage release-ceasefire deal was reached last month, Hamas and its allies have also repeatedly called the war a “victory” for their cause.

Indeed, Abu Marzouk’s remarks were quickly countered by Hamas spokesman Hazem Qassem, who said: “The occupation’s aggressive and destructive behavior is the cause of the destruction in Gaza. The October 7 epic marks a strategic turning point in the Palestinian national struggle.”

In a statement issued a short while later by the group itself, Hamas claimed Abu Marzouk’s comments were “incorrect and taken out of context.”

“The interview was conducted a few days ago and the published statements did not reflect the full content of the answers,” the terror group contended.

In the interview, Abu Marzouk said Hamas’s survival, despite Israel’s campaign in Gaza, constituted a “kind of victory.” He compared the terror group, which has been the de facto government of Gaza since ousting the Palestinian Authority’s main Fatah faction in a 2007 coup, to a regular person who has survived a boxing match with heavyweight champion Mike Tyson. But he said that in absolute terms, it would be “unacceptable” to call the war a win for the terror group.

“We’re talking about a party [Israel] that lost control of itself and took revenge against everything,” Abu Marzouk claimed. “That is not a victory under any circumstances.”
 
Hakuna anayejuta ni sawa na kusema Mkwawa alijuta kupigana na wakoloni kisa walitutandika. Au kusema Mandela alijuta kupigania uhuru kisa makaburu walimfunga miaka zaidi ya 20!!

Nchi zozote unazoona zipo huru **** struggle nyingi sana zilifanyika na mamilioni kufa. Mfano ni South Sudan, Eritrea n.k minorities walipigwa sana na kuchakazwa ila hatimaye wakapewa uhuru wao.

Zaidi tu ni kwamba hamas itapata wanachama wengi zaidi ambao watataka kulipa kisasi kwa hiki walichofanyiwa na Israel. Huwezi kujuta kupigania haki yako, hata hao Israel walipigania uhuru wao licha ya kuchinjwa na Hitler kama kuku na leo wakapata nchi yao!! Vipi nao walijuta?

So ni muoga tu hujuta kupigania haki. Ila uhuru wao ni suala la muda tu.
 
Shida moja ambayo hamsemi wakati ikiitwa palestina territory ndani yake kulikuwa na waarabu, wayahudi, wasamaria, druze, na mabedui. So tofauti ya hao akina mkwawa na mandela nk wao walikuwa wanapigana na wavamizi, hawa wanapigania kumiliki eneo lao wote. Maana kwa mfano angekuwa anatawala hapo mwarabu hao wayahud wasingefukuzwa maana kuna wayahud wenyeji ukiachia waliokuja kutoka ulaya , afrika, na uarabuni, au irani.
 
Hakuna anayejuta ni sawa na kusema Mkwawa alijuta kupigana na wakoloni kisa walitutandika. Au kusema Mandela alijuta kupigania uhuru kisa makaburu walimfunga miaka zaidi ya 20!!

Nchi zozote unazoona zipo huru **** struggle nyingi sana zilifanyika na mamilioni kufa. Mfano ni South Sudan, Eritrea n.k minorities walipigwa sana na kuchakazwa ila hatimaye wakapewa uhuru wao.

Zaidi tu ni kwamba hamas itapata wanachama wengi zaidi ambao watataka kulipa kisasi kwa hiki walichofanyiwa na Israel. Huwezi kujuta kupigania haki yako, hata hao Israel walipigania uhuru wao licha ya kuchinjwa na Hitler kama kuku na leo wakapata nchi yao!! Vipi nao walijuta?

So ni muoga tu hujuta kupigania haki. Ila uhuru wao ni suala la muda tu.
Ingekuwa upo shule ningekupa max zero... unatoa mifano isiyo endana na mada husika.

Pia Israel haijawahi pigana na hitller walistukizwa tu kwasababu ya chuki ya utajili wao na maendeleo ya haraka kwa vizazi vyao yaani hata watoto wa kiyahudi walikuwa wanageuka matajiri kwa muda mfupi.

Nimekupatia maneno ya Hamas wao wenyewe unapinga hivi mkoje raia wengine akili zenu... mna mahaba na Hamas hadi wao wanashangaa... Ile October 7 kuna makundi mengi mno na individuals walikuwa wanawatetea Hamas kwa vitendo walivyotena kichekesho Hamas wakawa wana post unyama wao lakini jamaa wanawatetea tu.. Yule mjinga wa UN alipoona noma akasema oh October 7 ilisababishwa miaka mingi ya nyuma huku hajui History ya Gaza 2005 kama Israel iliwapa PA ya Arafat Gaza.

Watumwa wa Allah na Hamas mmegeuka kinyaa
 
Well, mbona hawa Hamas wa Tabata Sanene kutwa kucha wanadai Hamas ndo imeshinda vita na kwamba yule jamaa aliyepanga shambulizi la Oktoba 7, yule ambaye alifumuliwa komwe na IDF, Yahya Sinwar, ni shujaa 🤣.

Mimi nashangaa tu! Shujaa gani kilaza namna ile?

Shujaa gani huyo aliyeshindwa kupima madhara ya majibu ya Israel?

Watu zaidi ya 45,000 wameuliwa. Vita imesababisha watoto wakiwa wengi kupita maelezo.

Gaza kimebaki kifusi tu.

Hiyo vita ambayo Hamas imeshinda, ni vita ipi?

Maana hata Waarabu wenzao wengi hawawaungi mkono.

Hakika majuto ni mjukuu. Waliobaki ndo wanaona upumbavu wa hilo shambulizi la Oktoba 7.

Hamas wote, wale wa Gaza na hata hawa wa Tabata Sanene, ni mazuzu.
 
Makobaz hata uyapige yatokwe damu sikioni bado yatarudia tu, tatizo dini.
 
So tofauti ya hao akina mkwawa na mandela nk wao walikuwa wanapigana na wavamizi,
Kasome vizuri historia, Mkwawa mbona aliwahi pigana na makabila mengine. Ile vita haikuwa ya kitaifa as a fact kama mkwawa angeshinda basi angetamua ufalme wake na kuwapiga majirani.
 
Pia Israel haijawahi pigana na hitller
Vijana hamjui historia, mbona kuna Brigade za wayahudi zilianzishwa kabisa kwenye jeshi la UK, US na Canada WW2. Pia huko Poland kuna resistance force ya wayahudi ilianzishwa ila ilichakazwa na Hitler je walijuta? HAPANA.... maana walijua wanapigania a just cause na mwishowe ikazaa uhuru wao.
Nimekupatia maneno ya Hamas wao wenyewe unapinga hivi mkoje raia wengine akili zenu.
Hizo ni unverified sources, huwezi okota maoni ya mtu mmoja ukatafanya ya taasisi. Hivi si Hamas hao hao juzi tu wamekiuka masharti ya cease fire? Kama walijuta wangeweza chezea cease fire?
Watumwa wa Allah na Hamas mmegeuka kinyaa
Hapa ndio mnakosea, mimi ni mkristo tena mlokole unaweza soma thread history yangu. Lakini nawaunga mkono Hamas kama tu Nyerere na Mandela walikua wakristo ila waliunga mkono Hamas for purely humanitarian reasons sio udini. Kwahiyo usilazimishe udini kwenye hili suala, ndio maana hata Gwajima hajaunga mkono huu uvamizi licha ya kwamba ni hard-core Christian.
Ile October 7 kuna makundi mengi mno na individuals walikuwa wanawatetea Hamas kwa vitendo walivyotena kichekesho Hamas wakawa wana post unyama wao lakini jamaa wanawatetea tu
Ndio hata Ukraine huwa wanapost wanavyowapiga warusi, na bado wanatetewa na dunia nzima. Sababu gani? Ukraine anapigania uhuru wake ila cha ajabu Hamas akipigania uhuru wake eti mchokozi? Hivi kwani Israel angeheshimu mipaka ya 1967 kuna tisasi ingerushwa? Mbona kule westbank hakunaga magaidi ila bado mnawaua kila siku?
 
Makobaz hata uyapige yatokwe damu sikioni bado yatarudia tu, tatizo dini.
We ndio unajua ukweli sasa, yaani huu ni mwanzo tu watarudia tena na tena mpaka uhuru kamili upatikane. Mnataka mumkalie mtu kimabavu alafu acheke tu?
 
Shujaa gani huyo aliyeshindwa kupima madhara ya majibu ya Israel?
Hivi mbona Mandela tunamuita shujaa ilihali alikua anafanya ugaidi wa kulipua majengo ya wazungu hadi akafungwa maisha? Nadhani anasifiwa kwa audacity maana licha ya odds kuwa against Hamas ila bado ali dare kutokusurrender kwa wavamizi. Same to mkwawa, mau mau, ANC wote walipigana na majeshi yenye nguvu mara elfu ila tunawaita mashujaa sababu walikataa kuwa makondoo mbele ya silaha za wazungu.
Watu zaidi ya 45,000 wameuliwa. Vita imesababisha watoto wakiwa wengi kupita maelezo.
Ukraine wamekufa zaidi ya hao ila humu wengi akiwemo wewe mnawasupport kujitetea, kwahiyo ulitaka zelensky naye akubali tu kuachia ardhi yake kwa Russia ili kuogopa madhara ya Russia? Hivi how cowardice is this view.
Gaza kimebaki kifusi tu.
Gaza kimebaki kifusi tu.
Hayo ni madhara ya vita, hata Syria imebaki magofu so is Libya. Vita yoyote huwa inakua hivyo whether uko upande wa haki au ubaya majengo yatavurugwa tu. Ni sawa na kusema Nyerere alikosea kupigana na Amin kisa tu uchumi wetu ulivurugwa na ile vita?
Maana hata Waarabu wenzao wengi hawawaungi mkono.
Of course hawawaungi kivipi, resolutions za UN lini kura za waarabu zilisupport Israel? Au support ulitaka ya kuwapa silaha? Geopolitics za Iran na Saudia ndio zinazowagawa ila hakuna muislam au muarabu timamu anaweza side na Israel instead of palestina.
Hakika majuto ni mjukuu. Waliobaki ndo wanaona upumbavu wa hilo shambulizi la Oktoba 7.
Hakuna anayejuta maana walikua na sababu ya kupigana. Mfano kule westbank mbona hakuna magaidi ila bado wapalestina wanauwawa kila siku bila sababu. Msitafute justification ya kutetea ukatili wa Israel ndio maana kule westbank jamaa hawarushi risasi ila kila siku watu wanaporwa nyumba na kuuwawa. Sasa hapo ukiamua kupigana utajuta kwa kipi? Maana hata usipopigana bado tu utateswa.

Nilichogundua humu watu wengi wanatawaliwa na udini tu. Ila Russia na Israel wanafanya kitu kimoja ila cha ajabu watu wanaona Israel ana haki ila Russia hana!! Insanity
 
Kasome vizuri historia, Mkwawa mbona aliwahi pigana na makabila mengine. Ile vita haikuwa ya kitaifa as a fact kama mkwawa angeshinda basi angetamua ufalme wake na kuwapiga majirani.
Kila kabila by then ni taifa ujue. So alipigana na taifa jiran.
 
Vijana hamjui historia, mbona kuna Brigade za wayahudi zilianzishwa kabisa kwenye jeshi la UK, US na Canada WW2. Pia huko Poland kuna resistance force ya wayahudi ilianzishwa ila ilichakazwa na Hitler je walijuta? HAPANA.... maana walijua wanapigania a just cause na mwishowe ikazaa uhuru wao.
Ungejua Historia ungekuwa na akili vizuri.. mimi nimezungumzia Israel wewe unazungumzia vikundi vya kiyahudi katika Vita ya Dunia hiyo time hata wazo la kufufua Israel halipo... acha kulewa pombe muda wote inakusumbua huelewi hata mada. Israel ni mchanganyiko wa makabila 12 ya Israel unapoongelewa Jew ni one tribe.. unahitaji shule ili uwe great thinker
Hizo ni unverified sources, huwezi okota maoni ya mtu mmoja ukatafanya ya taasisi. Hivi si Hamas hao hao juzi tu wamekiuka masharti ya cease fire? Kama walijuta wangeweza chezea cease fire?
Hamas kinachowaponza ni kusikiliza majinga kama nyinyi nje ya uwanja wanaleta ujeuri mziki wa Netanyahu hata ukileta utani anakupasua hapo hapo... this time hakuna upuuzi kuachwa mshaambiwa mtaondolewa hapo na ndicho kifuatacho IITV tambua hilo.
Hapa ndio mnakosea, mimi ni mkristo tena mlokole
Your not christian wewe... kasome upya biblia... hao Hamas ni same na Amarek God aliagiza wamalizwe so kama upo nao your on same boat with evil... ila fahamu kuwa they don't like you hata ufanyeje.... hata Trump alishatambua hilo kasikilize mahojiano yake anasema wazi kabisa this people haswa Muslims they don;t like us... wanajipenda wenyewe na Allah wao jipendekeze uwape hata taco hawatokupenda hahahahaha
unaweza soma thread history yangu. Lakini nawaunga mkono Hamas kama tu
Endelea tu Mr. Devil ila hamtokuja kamwe kuwin against Israel or Christians even Quran inatambua hilo
[61:14] O you who believe, be GOD’s supporters, like the disciples of Jesus, son of Mary. When he said to them, “Who are my supporters towards GOD,” they said, “We are GOD’s supporters.” Thus, a group from the Children of Israel believed, and another group disbelieved. We helped those who believed against their enemy, until they won.
يَـٰٓأَيُّهَا ٱلَّذِينَ ءَامَنُوا۟ كُونُوٓا۟ أَنصَارَ ٱللَّهِ كَمَا قَالَ عِيسَى ٱبْنُ مَرْيَمَ لِلْحَوَارِيِّـۧنَ مَنْ أَنصَارِىٓ إِلَى ٱللَّهِ قَالَ ٱلْحَوَارِيُّونَ نَحْنُ أَنصَارُ ٱللَّهِ فَـَٔامَنَت طَّآئِفَةٌ مِّنۢ بَنِىٓ إِسْرَٰٓءِيلَ وَكَفَرَت طَّآئِفَةٌ فَأَيَّدْنَا ٱلَّذِينَ ءَامَنُوا۟ عَلَىٰ عَدُوِّهِمْ فَأَصْبَحُوا۟ ظَـٰهِرِينَ
[3:55] Thus, GOD said, “O Jesus, I am terminating your life, raising you to Me, and ridding you of the disbelievers. I will exalt those who follow you above those who disbelieve, till the Day of Resurrection. Then to Me is the ultimate destiny of all of you, then I will judge among you regarding your disputes.
إِذْ قَالَ ٱللَّهُ يَـٰعِيسَىٰٓ إِنِّى مُتَوَفِّيكَ وَرَافِعُكَ إِلَىَّ وَمُطَهِّرُكَ مِنَ ٱلَّذِينَ كَفَرُوا۟ وَجَاعِلُ ٱلَّذِينَ ٱتَّبَعُوكَ فَوْقَ ٱلَّذِينَ كَفَرُوٓا۟ إِلَىٰ يَوْمِ ٱلْقِيَـٰمَةِ ثُمَّ إِلَىَّ مَرْجِعُكُمْ فَأَحْكُمُ بَيْنَكُمْ فِيمَا كُنتُمْ
Nyerere na Mandela walikua wakristo ila waliunga mkono Hamas for purely humanitarian reasons sio udini.
Nahisi wewe ni mwezi mchanga... Nyerere na Mandela waliwaunga mkono Hamas? vichaa wanaficha madhambi yao kwa Arabs Palestina na Hamas... kanuni za Hamas zinasema Israel iwe wiped out ndicho Nyerere na Mandela walichokuwa wanaunga mkono? go back to school and learn again yaani ukajirefresh bongo
Kwahiyo usilazimishe udini kwenye hili suala, ndio maana hata Gwajima hajaunga mkono huu uvamizi licha ya kwamba ni hard-core Christian.
Kumbe fuasi la Gwajima hahahahaha Gwajima ni wale waliogeuza Kanisa kuwa Pango la wezi Yesu alishawazungumzia... huna hoja.. and Gwaji wajua alikuwa akiitwa Rashidi?
Ndio hata Ukraine huwa wanapost wanavyowapiga warusi, na bado wanatetewa na dunia nzima. Sababu gani? Ukraine anapigania uhuru wake
Ukraine hapiganii Uhuru kilaza wewe jf imekumbwa na ugonjwa gani ?
ila cha ajabu Hamas akipigania uhuru wake eti mchokozi?
So Hamas ni watakatifu eti fanatic muslims wewe... i think umezaliwa yesterday so huna akili kanyonye mazima ya maza ako
Hivi kwani Israel angeheshimu mipaka ya 1967 kuna tisasi ingerushwa?
Ukitana Historia ya 1967 uliza nikupe viziri nadhani umelishwa matango pori... Kwa Taarifa yako after UN kuweka hiyo mipaka Israel akakubali tena eneo la Israel lilikuwa na wingi wa jangwa tena hakioti kitu na aliweza kulibadilisha likawa green yaani msitu mnene...

Arabs Country walikataa hiyo mipaka wakaivamia Israel ili wawamalize Genocide ambayo hawataki hata kuiongelea wanaishia kusema mipaka.. Israel aliwadunda mbaya sana... akawafurumusha na angetaka kuwafanyia kama wao walivyopanga kusingekuwa na ugomvi wowote unaoendelea kosa kubwa sana Israel alifanya kuwaonea huruma arabs akawaacha sasa mabichwa yamevimba mnapiga kelele
Mbona kule westbank hakunaga magaidi ila bado mnawaua kila siku?
Kwa kuwa umezaliwa jana kasome terrors in West bank against Israel na ili ujue why vifaru vipo west bank now dawa ya ugaidi ndio hii fukuza wote
 
Back
Top Bottom