Ni huzuri kuona wanadamu wa pande zote mbili wanakufa, bila kumpokea Mwokozi wa ulimwengu huu, that means wanaenda moja kwa moja jehanum ya moto. Mungu wetu, Mungu wa kweli hafurahii kifo cha mwenye dhambi, hata kama sisi tutafurahia kwamba gaidi au mwizi au mchawi kafa, Mungu hafurahii, anatamani kila mmoja wetu atubu asafishwe moyo ili kama akifa basi akaurithi uzima wa milele au kama ataendelea kuishi aishi akiwa mikononi mwa Mungu, sio mikononi mwa Ibilisi.
Imagine, 6,000 wote wamekufa wakiamini imani ya uongo kabisa, ya mungu baal, mungu wa kiarabu asiyeweza kuokoa hata unywele tu, na kwa wayahudi, wote waliokufa iwe kwa october 7 au wakati wa vita, hawamwamini Yesu Kristo, wanaishi kwa kufuata matendo ya mwili (kama tu wafanyavyo wasabato), wamesahau kuwa kwa matendo ya mwili (sheria) hapana mwenye mwili atakayempendeza Mungu, tumeokolewa kwa neema na sio kwa kujitahidi kufanya matendo mema kwa nguvu zetu, ajabu yake, Mungu ameleta mlango wa neema, lakini watu bado wanakimbilia mlango wa kuhesabiwa haki kwa matendo ya sheria, ambako tulishashindwa hadi Mungu akaunda mlango wa Neema, ni neema tu ya Mungu tunashinda dhambi, na pale tunapokosea tukirejea kwake kwa kutubu kwa kumaanisha kuacha dhambi anatusamehe na tunakuwa wasafi tena.
nawasihi nyote mtakaosoma hapa, kama haujaokoka jua kuwa siku yeyote ukifa unaenda moja kwa moja motoni, wokovu umeletwa kwa hiari, uchague uzima au mauti, vyote vipo mbele yako, kwa kuwa "Ukimkiri Yesu kwa kinywa chako ya kuwa ni Bwana, na kuamini moyoni mwako ya kuwa Mungu alimfufua katika wafu, utaokoka. Kwa maana kwa moyo mtu huamini hata kupata haki, na kwa kinywa hukiri hata kupata wokovu"(Rum. 10:9-18).
Unachotakiwa kufanya ni kumkiri ukimaanisha sasa kumpa maisha yako ayaongoze, yeye atakupatia Roho Mtakatifu ambaye atakuongoza uishi maisha masafi na utakuwa na uhakika wa uzima wa milele. pia itakupasa ujiunge na watu wenye imani sawa na wewe, imani ya wokovu ili uukulie wokovu. wengi huwa wanakuwa wabishi hadi siku wakikamatika na magonjwa au hatari fulani wanakumbuka shuka kukiwa kumeshakucha. 2 Wakorintho; inasema, Kwa maana asema, wakati uliokubalika nalikusikia, siku ya wokuvu nalikusaidia; tazama, wakati uliokubalika ndio sasa; tazama siku ya wokovu ndio sasa. usiseme nitaokoka kesho, okoka leo, kwasababu hujui utakufa kifo cha ghafla ukaenda mautini na mapombe yako, na uzinzi wako na dhurma zako n.k, kifo hakipigi hodi, wengine wanaamka asubuhi na mipango kibao, wanafika barabarani wanagongwa na kufariki hata kabla hawajasema Mungu nisamehe dhambi, hivyo wanaenda nazo.
Mvuvi mmoja aliyewahi kuwa mwanafunzi wa Yesu, mtu asiye kuwa na kisomo baada ya kushukiwa na Nguvu za Mungu, wayahudi walimwuliza, tufanye nini sasa?
Matendo 2:38 - 39 Petro akawaambia, Tubuni mkabatizwe kila mmoja kwa jina lake Yesu Kristo, mpate ondoleo la dhambi zenu, nanyi mtapokea kipawa cha Roho Mtakatifu. Kwa kuwa ahadi hii ni kwa ajili yenu, na kwa watoto wenu, na kwa watu wote walio mbali, na kwa wote watakaoitwa na Bwana Mungu wetu wamjie.
Kama una uhitaji wa kumpokea Yesu hata sasaivi uokoke, sali sala hii pamoja na mimi: Sema,
EE MUNGU MUUMBA WA MBINGU NA NCHI, MUNGU WA IBRAHIM ISAKA NA YAKOBO, NAKUJA KWAKO KWA NJIA YA KAFALA LA KIFO CHA YESU KRISTO MSALABANI, MBELE ZAKO MIMI NI MWENYE DHAMBI (ZITAJE KAMA UNAZIKUMBUKA), NAAMINI MOYONI MWANGU KWAMBA YESU KRISTO ALIKUFA KWA AJILI YA UKOMBOZI WANGU, NINAOMBA UNISAMEHE DHAMBI ZANGU ZOTE, UFUTE JILA LANGU KATIKA KITABU CHA HUKUMU, ANDIKA JINA LANGU KATIKA KITABU CHA UZIMA, NINAMKIRI YESU KRISTO KUWA BWANA NA MWOKOZI WA MAISHA YANGU KUANZIA SASA, NAOMBA UNIPATIE KIPAWA CHA ROHO MTAKATIFU ANIONGOZE, KUANZIA SASA MIMI NI MALI YAKO. KWA JINA LA YESU KRISTO, AMEN.
kama umeomba sala hii kwa kumaanisha moyoni mwako, sasa umeokoka, umesamehewa dhambi zako zote, na wewe ni mali ya Yesu Kristo, tafuta watu wenye imani sawa na wewe ujiunge nao ili ufundishwe wokovu, ukikosea tubu dhambi, endelea na maisha ya wokovu. Mungu akubariki.