Kufuatia kukamilika kwa mchakato wa utambulisho na Taasisi ya Kitaifa ya Tiba ya Uchunguzi kwa kushirikiana na Polisi wa Israeli, wawakilishi wa IDF wamefahamisha familia ya Bibas kwamba wapendwa wao, Ariel na Kfir Bibas miili yao imetambuliwa.
Kulingana na tathmini zilizofanywa na wataalamu, kulingana na taarifa za kijasusi zinazopatikana kwetu na matokeo ya kitaalamu kutoka kwa mchakato wa kuwatambua, Ariel na Kfir Bibas waliuawa kikatili wakiwa wanashikiliwa mateka na magaidi mnamo Novemba 2023.
Wakati wa mchakato wa utambulisho, ilibainika kuwa maili wa Mama yao uliopokewa jana si wa Shiri Bibas na si wa mateka mwingine yoyote. Hili ni kulingana na vipimo vya kitaalamu.
Huu ni ukiukwaji mkubwa wa shirika la kigaidi la Hamas, ambalo, kulingana na makubaliano, linalazimika kuwarudisha mateka wanne waliowauwa. Tunadai Hamas warejeshe mwili wa SHIRI BIBAS pamoja na mateka wetu wote.
Ariel Bibas, mwenye umri wa miaka minne wakati wa kifo chake, na Kfir Bibas, mwenye umri wa miezi kumi wakati wa kifo chake, walitekwa nyara pamoja na mama yao, Shiri Bibas, kutoka nyumbani kwao huko Nir Oz. Yarden Bibas, baba wa familia, alitoka kuwatetea naye alitekwa nyara mbele ya Shiri na watoto.
Yarden ilirejeshwa kama sehemu ya makubaliano ya kuachiliwa kwa mateka mnamo Februari 1, 2025. Magaidi wanaendelea kuchezea moto na ukiwaunguza dunia isilalamike kuwa wana one wa!!!
Tunashiriki katika huzuni kubwa ya familia ya Bibas katika wakati huu mgumu na tutaendelea kufanya kila juhudi kumrudisha Shiri na mateka wote nyumbani haraka iwezekanavyo.-Msemaji wa IDF