Hamas waliobakia wanapaswa kutumia hii fursa ya kuachiliwa mateka na wao kujisalimisha, wasisubiri kuangamizwa!

Hamas waliobakia wanapaswa kutumia hii fursa ya kuachiliwa mateka na wao kujisalimisha, wasisubiri kuangamizwa!

Zanzibar-ASP

JF-Expert Member
Joined
Nov 28, 2013
Posts
11,550
Reaction score
40,697
Ni fursa adimu sana jeshi la Israel limetoa la kusimamisha vita kwa siku chache ili kupisha zoezi la kubadilishana mateka na kuruhusu misaada ya kibinadamu kuingiza Gaza kabla ya zoezi la mashambulizi mazito kuendelea mbele ili kuhakikisha hakuna punje inayoitwa Hamas inabakia Gaza.

Kama Hamas wana akili timamu na wale wote wanaowaunga mkono Hamas huku wakiwatakia mema wapalestina wote, huu ndio muda muafaka zaidi wa kutumia fursa ya kuwaokoa wapalestina wote kutoka kwenye mwendelezo wa kipigo kizito kutoka kwa jeshi la Israeli kwa kuamua kujisalimisha.

Mimi sipendi vita.
Mimi sipendi kabisa kuona damu za wapalestina zinaendelea kumwagika kisa Hamas.
Bora Hamas ikajisalimisha kuepusha maafa kwa wapalestina wengi zaidi.

HERI NUSU SHARI KULIKO SHARI KAMILI.
 
Kwahiyo kwa akili yako unaamini kwamba Hamas itafutwa kabisa?

Hamas ni Palestina na Palestina ni Hamas. Kwanza wamepata umaarufu zaidi kwa wananchi wao. Haswa baada ya Israel kuamuwa wajadiliane kuachia mateka wakati walisema hawezi kujadiliana nao zaidi ya kuwaangamiza na kuwaokoa mateka.

Kuifuta Hamas ni lazima waifute Palestine yote.

Mark this post nitarudi hapa kukuuliza. Kwani vita imeisha?

Solution ni a two state side by side kurudi kwenye mipaka ya UN at least 1967.
 
Hamas is an idea. You can’t kill an idea with a barrel of the gun.
 
Uharo wa Bata huu. Uchaguzi 2025 pigania katiba mpya ya hamas yaache. Hamas wanapigania nchi yao.
 
kabla ya zoezi la mashambulizi mazito kuendelea mbele ili kuhakikisha hakuna punje inayoitwa Hamas inabakia Gaza.
Hauko serious, kwa hii vita tu kuna wapalestina maelfu watajiunga Hamas tena na tena. Violence haimalizwi kwa violence
 
Hamas hatuwajui, na Gaza hatuijui na vita yao hatuijui, wapalestina wanapata mahitaji kama umeme na maji toka Israel, bora tuwaachie wenyewe vita yao maana Israel wamesema wanacontrol Gaza ila mateka wao wameachiwa katikati ya Gaza City! Na Israel hawajui mateka wao wengine walikofichwa!

Vifaru na magari ya Israel vimetelekezwa baada ya askari wao mamia kuuwawa Gaza City wao wamesema eti ni 70 tu na vita ya ardhini Gaza City haioneshwi , hatujui wanauwawaje , hapo utajua hujui!

Hamas Iko supported na Iran, Lebanon, Qatar na Egypt wale hawataisha kamwe maana Hamas wengine wengi wako nchi zingine!
 
Cha kwanza Israel inataka kuharibu base yao kabisa ukanda wa Gaza. Hawa jamaa waliweka base hadi ndani ya hospital. Bomoa mahandaki yote. Ukitaka kuondoa panya haribu maficho yake kwanza.

Hii vita Israel inajua ni endelevu na wameshasema itachukua muda mrefu. Chunga hiyo kauli ya itachukua muda mrefu.

Nalaani kitendo cha Hamas kuivamia Israel na masquad ili kuizamisha ardhini. Hali hiyo imepelekea malipizi kwa Wapalestina pia wasio na hatia.
 
Back
Top Bottom